- Maseneta wamekuwa wakilalama kuhusu kupuuzwa na wabunge
- mzozo huo ulionekana mwanzoni kama mapigano ya maamlaka
Mahakama kuu imefutilia mbali miswada 23 iliyopitishwa na bunge bila kulihusisha bunge la senate .
Jopo la majaji watatu siku ya alhamisi limeamuru kwamba spika wa bunge anafaa kumhusisha mwenzake wa senate .
“ sheria hizo tata zinakiuka vipengee vya 96,109,110,111,112 na 113 vya katiba na hivyo ni ukiukaji wa katiba’Majaji hao wameamuru .
Baadhi ya miswada ambayo imeathiriwa ni ule wa kompyuta na kukabiliana na uhalifu wa mtandaoni na ule wa Fedha wa mwaka wa 2018 .
Katika kesi hiyo senate ilikuwa imewasilisha kesi kortini kupinga uamuzi wa wa bunge kupitisha miswada hiyo bila mchango wa maseneta .
kuhusu gharama ya kuifutilia mbali miswada hiyo majaji wamesema bunge lingefikiria kwanza kuhusu kupitisha misawada hiyo bila mchango wa senate .
bunge la kitaifa lilikuwa limesema kwamba kuifutilia mbali misawada hiyo ni hatua itakayosababisha hasara kubwa kwa serikali kwa sababu ya gharama yake .
Mahakama pia imesema kwamba marekebisho ya sehemu ya 4 ya sheria kuhusu ununuzi wa bidhaa za matibabu ni ukiukaji wa sheria na hivyo basi kinyume cha katiba .
Maseeta wamekuwa katika mzozo wa muda mrefu na bunge kuhusu wajibu wao katika masuala ya utayarishaji wa sheria .
Wamekuwa wakiwashtumu wenzao wa bunge la kitaifa kwa kuwapuuza na kuhujumu majukumu yao . bunge kwa upande wake limedai kwamba maseneta wanataka kujipa majukumu yasio yao kwa kufanya kazi sawia ni ile ya wabunge