Kipruto amekanusha mashtaka hayo dhidi yake

Bingwa wa Olimpiki Conseslus Kipruto aachiliwa kwa dhamana katika kesi ya kumdhulumu kingono msichana wa miaka 15

Wakaazi walianfamana nje ya mahakama

Muhtasari

 

 Kipruto amefikishwa katikama mahakama ya  Kapsabet jumatatu asubuhi 

 Kesi itatajwa mei tarehe 20 mwaka ujao 

 

 

Bingwa wa mbio za Olimpiki  Conseslus Kipruto ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili baada ya kukanusha mashtaka ya kumdhulumu kimapenzi mischana mwenye umri wa miaka 15

 Mahakama ya Kapsabet imeelezwa kwamba Kipruto alitekeleza uhalifu huo  kati ya tarehe 20 na 21 mwaka huu katika Lokesheni ya  Tironin kaunti ya Nandi . Stakabadhi ya mahakama imeonyesha upande wa mashtaka una mashaidi  watoto dhidi ya Kipruto .

 Kesi hiyo itatajwa mei tarehe 20 mwaka  wa 20221 . Umati wa watu ulifurika nje ya mahakama kuandamana dhidi ya mwanariadha huyo .