Kiapo

Immaculate Kassait aapishwa kuwa Kamishna wa Data

Kassait anakuwa mtu wa kwanza kuishikilia nafasi hiyo

Muhtasari

 

  •  Uteuzi wake uliidhinishwa na bunge wiki jana 
  •  Kassait anakuwa mtu wa kwanza kuishikilia nafasi hiyo 
  •  Awali alikuwa akifanya kazi katika tume ya IEBC 

 

Immaculate Kassait  ameapishwa kuhudumu  kama kamishna wa data baada ya rais kuweka uteuzi wake katika gazeti rasmi la serikali .

Kassait  alikula kiapo   siku ya jumatatu katika afisi ya msajili mkuu  kwenye hafla iliyoongozwa na msajili wa mahakama ya juu zaidi Moses Serem .

 Kiapo hicho kilisimamiwa na  afisa kutoka afisi ya msajili mkuu wa idara ya mahakama Sharon   Mwayuli.

Kassait  atahudumu katika wadhifa huo mpya kwa muda wa miaka 6  baada ya kamati ya bunge kuhusu  ICT kuidhinisha uteuzi wake . Awali kabla ya kuteuliwa katika nafasi hiyo Kassait alikuwa mkurugenzi wa IEBC kuhusu usajili wa wapiga kura .

 Kamishna huyo wa data pia amewahi kufanya kazi katika  taasisi ya elimu na demokrasia na kama afisa wa mipango katika shirika la FIDA Kenya