SAHIHI ZA BBI

IEBC yatoa muundo wa kutumiwa kukuanya sahihi za BBI

Shughuli ya ukusanyaji wa sahihi itafanyika kwa siku zijazo

Muhtasari

 

  •  IEBC imeidhinisha muundo wa ukusanyaji wa saini 
  •  zoezi hilo litazinduliwa siku ya jumatano 

 

Tume  huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imetoa muundo wa jinsi sahihi za BBI  zitakavyokusanya kuanzia hapo kesho wakati zoezi hilo litakapozinduliwa

 Katika barua kwa kamati inayoongoza shughuli hiyo mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati  amesema wameidhinisha muundo utakaotumiwa wakati wa ukusanyaji wa sahihi hizo  ili kurekebisha katiba kupitia kura ya maoni .

  Barua hiyo  ilikuwa majibu ya barua iliyokua imeandikwa na kamati hiyo ikitaka idhini ya muundao unaofa kutumiwa .

 Kamati ya usimamizi wa mchakato wa BBI imesema kwamba inalenga kukusanya sahihi milioni katika kipindi cha wiki moja . zoezi hilo litafanyika kesho baada ya kuahirishwa  wiki jana .