- Kinoti amesema hakuna mpango wa kuzifufua kesi hizo
- Jana waathiriwa wa ghasia za 2007/08 walifurika makao makuu ya DCI kuandikisha taarifa
Mkurugenzi mkuu wa DCI George Kinoti amekanusha madai kwamba idara yake inalenga kuzifufua kesi za ghasia za uchaguzi za mwaka wa 2007/08 .
Kinoti siku ya jumanne amesema kikao chake siku ya jumatatu na wanahabari hakikulenga kumaanisha kwamba DCI ilikuwa ikizifufua kesi za ghasia za baada ya uchaguzi .
Amesema hatua hiyo ilitokana na na hofu kutoka kwa baadhi ya wakenya ambao walitaka kuhakikishiwa na DCI kwamba hapatatokea tena ghasia za uchaguzi na kwamba idara ya DCI itachunguza kesi zote za vitishoi dhidi ya wakenya .
Amesema wamepokea ripoti nyingi kuhusu wananchi ambao wanahofishwa na uwezekano wa kupoteza mali yao na kaisha yao kwa ajili ya vitisho wanavyopokea .
Ilikuwa imeripotiwa kwamba serikali imegeuza nia na sasa inataka kuzifufua tena kesi za ghaia za baada ya uchaguzi huo ikiwemo kisa cha mauaji ya watu katika kanisa la Kiambaa .
Hatua hiyo imejiri miaka saba baada ya serikali kufunga kesi hizo ikisema hakuna ushahidi wa kuwafungulia mashtaka waliotekeleza ghasia ,mauaji na uharibifu wa mali baada ya watu 1300 kufariki na Zaidi ya 650,000 kutoroka makwao .
Wiki tatu zilizopita wakili wa waathiriwa Paul Gicheru alijisalimisha kwa mahakama ya ICC hatua ambayo ilizua tumbo joto katika kambi ya naibu wa rais William Ruto na washirika wake wamedai kwamba hatua ya DCI ni muendelezo wa hila dhidi yake kumzuia kuchukua usukani wa serikali mwaka wa 2022 .
Kinoti baada ya kukutana na waathiria wa ghasia hizo waliofurika DCI kuandikisha taarifa alisema wamepokea ripoti 72 z amauji na 44 za mizozo ya mashamba huku kesi 118 za vitisho zikisajiliwa kuhusiana na ghasia za 2007/2008