Lawama

DCI Kinoti anatumiwa kumhujumu Ruto-Adai Sudi

DCI imesema inachunguza vitisho dhidi ya baadhi ya waathiriwa wa ghasia za uchaguzi

Muhtasari

 

  • Siku ya jumatatu DCI Kinoti ameapa kukabiliana na waliotekeleza ghasia za uchaguzi wa 2007/08
  • Siku ya jumatatu DCI Kinoti ameapa kukabiliana na waliotekeleza ghasia za uchaguzi wa 2007/08

 

 

   Mbunge wa  Kapseret Oscar Sudi amedai kwamba  mkurugenzi wa DCI George Kinoti anatumiwa na baadhi ya watu ili kumzuia naibu wa rais William Ruto kumritji rais Uhuru Kenyatta mwaka wa 2022 .

 Hii ni baada ya Kinoti kutangaza kwamba anazifufua kesi  dhidi ya watuhumiwa wa ghasia za  baada ya uchaguzi mkuu wa 2007/08

      Amedai kwamba Kinoti na baadhi ya  maafisa kutoka Ikulu na wizara ya usalama wa ndani ndio walio na njama ya kuzifufua kesi hizo  kwa lengo la kumzuia Ruto kusjhinda uchaguzi mkuu ujao . Sudi amesema Kinoti na maafisa hao ndiuo waliomtyuma wakili  Paul Gicheru kwenda ICC na pia kuna afisa mkuu wa polisi anayelengwa  kutumwa huko kama sehemu ya njama dhidi ya Ruto .

Sudi  amedai kwamba Kinoti na kundi lake  wamekuwa wakimtnga naibu wa rais kuhusu masuala ya serikali na wana hila ya kuzua tofauti kati ya rais Uhuru na naibu wake Ruto . Amesema kanisa la Kiambaa lililoteketezwa wakati wa ghasia hizo lipo katika eneo bunge lake na hakuna njama zitakazofaulu kuzifufua kesi hizo kwani hatua hiyo itazua uhasama na mgawanyiko miongoni mwa wakenya .