Maambukizi ya HIV

Watoto wa shule wanasheheni idadi kubwa ya maambukizi mapya ya HIV –NACC

visa vingIne vipya vya maambukizi 8.191 vilisajiliwa miongoni mwa walio na umri wa miaka kati ya 20-24

Muhtasari
  •  Takwimu za NACC  zaonyesha kwamba  visa 41,728 vipya vya maambukizi vilisajiliwa mwaka huu huku visa   25,062  vikiwa vya wasichana ilhali wavulana ni 16,666
  •  Data zaonyesha kwamba  visa vipya vya maambukizi 6,247 ni vya watoto walio na kati ya umri wa miaka 15-19 . kati ya visa hivyo 4,254 ni wasichana ilhali 993 ni wavulana

 

Watoto wa shule wanasheni sehemu kubwa ya maambukizi mapya ya HIV  kulingana na  takwimu za baraza la kupambana na HIV NACC . Wasichana wado ndio waathiriwa wakubwa wa ugonjwa huo .

 Takwimu hizo zimeonyesha kwamba mwaka huu pekee  visa vipya 21,404 vya  maambukizi ni vya watoto wanaoenda shule . Idadi hiyo ni  Zaidi ya jumla ya maambukizi ya HIV yaliosajiliwa kote nchini mwaka jana .

 Takwimu za NACC  zaonyesha kwamba  visa 41,728 vipya vya maambukizi vilisajiliwa mwaka huu huku visa   25,062  vikiwa vya wasichana ilhali wavulana ni 16,666

 Wale walio na umri wa miaka 15 na Zaidi ni 34,610 ilhali visa 6,806 ni vya wanafunzi walio na umri wa miaka 14 na chini .

Kisumu, Nairobi, Siaya, Homa Bay, Migori, Nakuru, Mombasa, Kisii, Kakamega  na  Kiambu  ni kaunnti zinazoshikilia kumi bora kwa idadi ya juu ya maambukizi mapya mwaka huu

 Data zaonyesha kwamba  visa vipya vya maambukizi 6,247 ni vya watoto walio na kati ya umri wa miaka 15-19 . kati ya visa hivyo 4,254 ni wasichana ilhali 993 ni wavulana .

 Kitengo hicho kinasheheni wanafunzi wa shule za msingi na Upili .

 Kwa mujibu wa takwimu hzo  visa vingIne vipya vya maambukizi 8.191 vilisajiliwa miongoni mwa walio na umri wa miaka kati ya 20-24 . kati yao 5,166 ni wasichana ilhali 3,014 ni wavulana katika vyuo vikuu na taasisi za  elimu ya juu