Covid 19

5 zaidi wafariki huku 551 wakipatikana na Corona

Nairobi inaongoza kwa visa 212 ,kilifi ina visa 39 ilhali Mombasa ina visa 35.

Muhtasari
  •  Idadi ya watu waliofariki kwa ajili ya virusi hivyo imeongezeka hadi 1,474 baada ya watu 5 kuaga dunia .
  •    Wagonjwa  Wengine  266 wamepona ugonjwa huo   na kufikisha 55,610 idadi ya waliopona ugonjwa huo hadi kufikia sasa.

 

CAS wa Afya Rashid Aman

Kenya leo imesajili visa vipya 551 vya corona baada ya sampuli 4,675 kupimwa na kufikisha jumla ya visa hivyo kufika 84,169 ,amesema katibu wa utawala wa wizara ya Afya Rashid Aman

 Idadi ya watu waliofariki kwa ajili ya virusi hivyo imeongezeka hadi 1,474 baada ya watu 5 kuaga dunia .

 Aman amesema kuna wagonjwa   1,275  katika hospitali mbali mbali nchini huku wengine 8,070 wakiwa chini ya utunzi wa nyumbani . wagonjwa 71 wapo katika kitengo cha ICU   huku 18 wakiwa katika kitengo cha HDU

   Wagonjwa  Wengine  266 wamepona ugonjwa huo   na kufikisha 55,610 idadi ya waliopona ugonjwa huo hadi kufikia sasa.

 Kutoka visa hivyo vipya  525 ni wakenya ilhali 26 ni raia wa kigeni  .wagonjwa 301 ni wanaume huku wanawake wakiwa 250 .Mgonjwa wa umri wa chini  ni mtoto wa siku saba ilhali wa umri wa juu ana miaka 100 .

Nairobi  inaongoza kwa visa 212 ,kilifi ina visa 39 ilhali Mombasa ina visa 35.