- Wahome kupitia taarifa amesema BBI ni njama inayolenga kumweka Uhuru madarakai hata wakati kipini chake afisini kitakapokamilika mwaka wa 2022 .
- Amewaonya wakenya kwamba watajutia Iwapo marakebisho ya katiba yanayopendekezwa na Uhuru na kiongozi wa ODM Raila Odinga yatapitishwa .
Mbunge wa kandara Alice Wahome kwa mara nyingine tena amemshambulia rais Uhuru Kenyatta kwa kutumia BBI kama njia ya kusalia madarakani baada ya muhula wake wa pili kutamatika .
Mbunge huyo siku ya jumamosi alidai kwamba rais analenga kurekebisha katiba ya mwaka wa 2010 ili kumsaidia kuthibiti madaraka ya serikali akiwa nje ya uongozi .
Wahome kupitia taarifa amesema BBI ni njama inayolenga kumweka Uhuru madarakai hata wakati kipini chake afisini kitakapokamilika mwaka wa 2022 .
Amewaonya wakenya kwamba watajutia Iwapo marakebisho ya katiba yanayopendekezwa na Uhuru na kiongozi wa ODM Raila Odinga yatapitishwa .
“ Kwa Kenya kusalia nchi ya demokrasia ya kweli rais wetu anafaa kukubali kwamba hatamu yake inafika tamati .Anafaa kuhakikisha kwamba madaraka yanakabidhiwa mtu mwingine kwa njia ya Amani na aende nyumbani’ amesema Wahome .
Ameongeza ; ‘Hafai kuruhusiwa kuongeza muda wake madarakai kwa njia moja au nyingine’
Sio mara ya kwanza kwa Wahome kumshtumu rais Uhuru kwa kuwa na lengo la kusalia madarakani baada ya kutamatika kwa kipindi chake mwaka ujao .
Wahome, ambaye ni mshirika wa karibu wa naibu wa rais William Ruto pia amemtaja Uhuru kama tishio kubwa kwa demokrasia ya kikatiba ,ugatuzi na rais aliyesimamia kuvurugwa kwa uchumi wan chi katika miaka yake mitano uongozini .