Siasa

[Picha ] Gideon Moi azuiwa kufanya mkutano na wazee wa Talai

Baadaye alikutana na wazee hao lakini haijafahamika Iwapo sherehe hiyo ya kumpa Baraka itafanyika .

Muhtasari
  •  Msemaji wa Gideon  amethibitisha kwamba  kiongozi huyo wa KANU alikuwa katika eneo hilo baada y kualikwa na wazee wakiongozwa na Christopher Koyogi .
  •  Wazee hao mwaka jana walikutana na naibu wa rais William Ruto  na kumbpa Baraka  kama msemaji na kiongozi wa jamii ya wakalenjin .

 

 Seneta wa  Baringo Gideon Moi  siku ya jumamosi  alikutana na kundi la vijana waliozuia kundi lake  njiani kwenda katika mkutano wa alfajiri na wazee wa ukoo wa Talai huko Nndi .

 Wazee hao mwaka jana walikutana na naibu w arais William Ruto  na kumbpa Baraka  kama msemaji na kiongozi wa jamii ya wakalenjin .

 Mamia ya vijana waliziba  barabara zinazoelekea  Kapsisiywa  ambako Gideon  alikuwa amewaalika baadhi ya wazee kwa hafla ya kumpa pia Baraka  huku uhsama wa kisiaa kati yake na naibu wa rais William Ruto ukizidi  tunapolekewa  kwa uchaguzi mkuu wa mwaka wa ujao .

Gideon na kundi lake waliwasili katika eneo holo mwendo wa saa kumi alfajiri  katika msafara wa magari Zaidi ya manne  na ni katika  barabara ya Sangalo-kabiyet ambako msafara wao ulizuiwa  na  vijana walioiziba barabara  kwamba tayari wazee wa Talai walikuwa wameshampa Ruto Baraka za kuwa kiongozi wa jamii hiyo

 Msemaji wa Gideon  amethibitisha kwamba  kiongozi huyo wa KANU alikuwa katika eneo hilo baada y kualikwa na wazee wakiongozwa na Christopher Koyogi .

 Gideon  alilazimika kuwashawishi vijana hao kukoma kuzua rabha kwani alikuwa na haki kama mkenya yeyote kuzuru eneo hilo  .Baadaye alikutana na wazee hao lakini haijafahamika Iwapo sherehe hiyo ya kumpa Baraka itafanyika .