Moto

Mwanamume afariki katika mkasa wa moto Nyamira

Ameongeza kwamba wanakijiji walijaribu kuingia katika nyumba hiyo lakini wakagundua kwamba mlango ulikuwa umefungiwa ndani

Muhtasari
  • Waliuvunja mlango na kuingia ndani lakini wakati huo mzee huyo alikuwa ameshachomeka
  • Polisi  wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo

  

Nyumba ambapo mwanamme mmoja ameteketea hadi kufa ,Nyamira
Image: Alvin Ratemo

 Mwanamume mmoja ameteketea hadi kufa katika nyumba yake kijijini Nyankoba huko Nyamira .

 Kulingana na  naibu wa chifu wa eneo hilo  Eric Marando, Harrison Morori mwenye umri wa miaka 70 alichomeka  akiwa nyumbani kwake alikoishi peke yake.

" Iliripotiwa kwamba moto ulianzia katika sebule yake  ambapo majirani walikimbia kumuokoa  lakini hawakufaulu’ amesema naibu huyo wa chifu .

 

 Ameongeza kwamba wanakijiji  walijaribu kuingia  katika nyumba hiyo lakini wakagundua kwamba mlango ulikuwa umefungiwa ndani. Waliuvunja mlango na kuingia ndani lakini wakati huo mzee huyo alikuwa ameshachomeka. Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo