Serikali haitaruhusu shule kuwa na kiasi kikubwa cha sanitizer shuleni ,waziri wa elimu George Magoha amesema .
Magoha amesema ni lita tano pekee za sanitizer zitakazokubaliwa shuleni na zitahifadhiwa na walimu . Alizungumza hayo katika shule ya msingi ya Kiangochi siku ya jumamosi akifnya ukaguzi wa matayarisho ya kufunguliwa kwa shule . Alisema kemikali hiyo ina asilimia 70 ya pombe na inaweza kutumia vibaya na wanafunzi .
“ watoto wetu wana ubunifu sana na tunajua wanachoweza kufanya kutumia sanitizer . hatutaruhusu Zaidi ya litano tano za sanitizer katika kila shule’ amesema Magoha .
Pia aliongeza kwamba Zaidi ya maski milioni 7 zimetolewa kusambazwa kwa wanafunzi maskini kote nchini .