Magoha apiga marufuku ziara za wazazi shuleni

Muhtasari

  • Waziri Magoha alitangaza kwamba hakuna mzazi au wageni watakao ruhusiwa sheleni muhula huu.

  • Waziri alisema hii ni kwa sababu mitihani ya kitaifa itafanyika muhula huu.  

Waziri wa elimu George Magoha
Waziri wa elimu George Magoha Waziri wa elimu George Magoha

Waziri wa Elimu George Magoha siku ya Jumatano alitangaza kwamba hakuna mzazi au wageni wengine watakao ruhusiwa shuleni muhula huu.

Waziri alisema hii ni kwa sababu mitihani ya kitaifa itafanyika muhula huu.  

Vile vile Magoha alikemea vyombo vya habari kwa kutoa habari potovu kuhusu hali ya Covid-19 shuleni.

 
 

Magoha alishutumu vyombo vya habari kwa kuchapisha habari zinazoegemea upande mmoja.

Akiongea katika mkao wa wanahabari  mjini Nairobi wakati akikutana na wadau wa elimu Magoha alisema vyombo vya habari vilizingatia upande hasi tu bila kuonyesha mafanikio ambayo yamepatikana.

Kutokana na hali hii, waziri alisema hakuna mwanahabari au mzazi atakayeruhusiwa shuleni.

Alisema hii itawapa wanafunzi kote nchini wakati wa kutosha wa kuzingatia masomo yao bila matatizo.

Magoha alisema kwamba haamini tena vyombo vya habari.

"... udhaifu wangu ni kukuambia ukweli ili tusibishane juu yake. Una hata ujasiri wa kuchora katuni kunihusu lakini nataka kukujulisha kwamba  kama mtumishi wa umma naweza kuhimili mishale yote kwa sababu nina nguvu sana, " alisema.

Magoha alisema kwa mfano wizara inakaribia kumaliza Kikosi Kazi cha mtaala mpya wa CBC lakini waandishi wa habari wengine tayari wamekuwa wakiripoti kuhusu mambo ambayo bado hayajakamilika.

 

"Hiyo ni haki kwa watu katika taaluma yako kuripoti juu ya mambo ambayo hayajakamilika. Hakuna mtu aliye mkamilifu na sipaswi kukashifiwa kwa sababu sitafuti kazi bali ninawahudumia watoto tu," Magoha alisema.