Polisi kuchunguza kisa cha mwanamume aliyeaga dunia akifanya mapenzi na mpenzi wake

Muhtasari
  • Jamaa aaga dunia akifanya ngono na mpenzi wake Dandora kaunti ya Nairobi

Polisi eneo la Dandora kaunti ya Nairobi wanachunguza kisa kimoja ambapo mwanamme mmoja aliaga dunia akikula udora wa mpenzi wake, Januari 6.

Robert Maina, mfanyikazi wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alikuwa akila mahaba na mpenziwe aliyetambulika kama Joyce Wairimu Wangare wakati ghafla alishindwa kupumua na kukata roho.

Ripoti ya polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Dandora ilionyesha Wairimu aligutushwa na tukio hilo ambapo alikimbia kwenda kupiga ripoti.

Maafisa wa polisi walitembelea eneo la tukio na kumkuta Maina akiwa amelala kwenye kitanda.

"Alizimia na kuaga dunia papo hapo wakati wa kitendo hicho. Nyumbani kwake, kulipatikana na dawa na vile vile ripoti ya matibabu." Polisi walisema.

Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika makafani ya kuifadhani maiti ya City Mortuary.