Idara ya mahakama

Mwilu huenda akajipata pabaya katika kipute cha kumrithi Maraga

Mwilu ambaye ndiye kaimu rais wa mahakama ya juu Zaidi alionekana kuwa kifua mbele katika kinyang’anyiro cha kumrithi Maraga .

Muhtasari
  •  Duru zaarifu kwamba jaji wa mahakama ya juu Zaidi  Mohamed Ibrahim anatarajiwa kuchukua usukani kama kaimu jai mkuu .
  • Mwilu  ambaye ndiye kaimu  rais wa mahakama ya juu Zaidi alionekana kuwa kifua mbele katika kinyang’anyiro cha kumrithi Maraga .
Kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu baada ya kukabidhiwa mamlaka na David Maraga.
Kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu baada ya kukabidhiwa mamlaka na David Maraga.

 

 Kaimu  jaji mkuu Philomena Mwilu amepata pigo katika azma yake ya kutaka kumrithi mtangulizi wake  David Maraga . katika hatua moja mahakama kuu imefanya maamuzi manne ambayo yanatia hatarini uwezo wa  Mwilu kuichukua nafasi hiyo kwa njia ya kudumu .

 Mahakama kuu imetoa uamuzi wa kumuondoa Mwilu katika nafasi yake kama   naibu jaji mkuu ,mwanachama wa tume ya JSC  ,Jaji wa mahakama ya juu Zaidi na  msimamizi mkuu wa kuafikia haki katika idara ya mahakama .

 Hatua hiyo pia inamaanisha kwamba  Mwilu  atakoma kuhudumu kama kaimu wa jaji mkuu  na mwneyekiti wa tume ya JSC nafasi ambazo ni muhimu  alizochukua baada ya kustaafu kwa Maraga .

 Jaji  Patrick Jeremy Otieno  ndiye aliyetoa uamuzi huo siku ya ijumaa na  sasa hatua hiyo inamzuia Mwilu dhidi ya kuongoza vikao vya JSC  na hivyo basi kumbandua kutoka mchakato mzima wa kumtafuta jaji mkuu mpya .

 Duru zaarifu kwamba jaji wa mahakama ya juu Zaidi  Mohamed Ibrahim anatarajiwa kuchukua usukani kama kaimu jai mkuu .

Mwilu  ambaye ndiye kaimu  rais wa mahakama ya juu Zaidi alionekana kuwa kifua mbele katika kinyang’anyiro cha kumrithi Maraga .

 Uamuzi huo wa mahakama ulitolewa Meru  baada ya  Isaiah Mbiti kuwasilisha kesi kupinga kuwepo kwa Mwilu afisini kwa madai ya kutumia vibaya maamlaka ya afisi yake

 Mbiti alidai kwamba kuendelea kusalia kwa Mwili afisini huku akikabiliwa an kesi ya ufisadi ni mapendeleo na ukiukaji wa suta ya sita a katiba .