Matokeo

Matokeo mabaya shuleni huenda yakadhihirika katika KCPE,KCSE

Hi ni kwa sababu mtaala wa 8-4-4 na mtaala mpya inahitaji mazoezi ya kila mara ikiwemo kusoma na wanafunzi kutangamana darasani walimu .

Muhtasari
  • Wanafunzi walikuwa nyumbani  kwa miezi tisa  na wengine kwa miezi 10  huku wakikosa kabisa kutangamana na walimu au kuendelea na mazoezi ya kusoma
  • Wanafunzi katika maeneo ya mijini walikuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao  na vifaa vya elektroniki kama simu na vipakatalishi  ili kuendelea kusoma

 

Waziri wa elimu George Magoha

Kudorora kwa matokeo ya wanafunzi hakukutarajiwa  katika mitihan wa wanafunzi wa gredi ya nne na  darasa la nane bali  katika madarasa yote .

 Hi ni kwa sababu mtaala wa 8-4-4  na mtaala mpya  inahitaji mazoezi ya kila mara  ikiwemo kusoma na  wanafunzi kutangamana darasani walimu .

  Wanafunzi walikuwa nyumbani  kwa miezi tisa  na wengine kwa miezi 10  huku wakikosa kabisa kutangamana na walimu au kuendelea na mazoezi ya kusoma . Juhudi adimu za kuwafunza kupitia mtandao  ,redio au runinga hazikuweza kuziba mianya iliyoachwa baada ya shule kufungwa mwezi machi kwa ajili ya janga la Corona .

   Sababu hiyo ndio inayofanya pawepo pengo kubwa la matokeo kati ya wanafunzi katika maeneo ya mashambani na mijini .

  Wanafunzi katika maeneo ya mijini walikuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao  na vifaa vya elektroniki kama simu na vipakatalishi  ili kuendelea kusoma . Kudorora kwa matokeo yao huenda kukadhihirika katika matokeo ya mitihani ya KCPE  na KCSE  ambayo itaanza katika wiki chache zijazo .