TSC yahamishia huduma zake mtandaoni

Muhtasari

 • Hapatakuwepo maombi ya moja kwa moja ya uajiri na upandishaji ngazi walimu kuanzia Machi Mosi.

 • Maombi ya uhamisho yatapatikana kupitia tovuti ya Tume katika www.tsc.go.ke

Afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia
Mkuu wa TSC Nancy Macharia Afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia

Upandishaji ngazi na uhamishaji wa walimu sasa utafanywa mtandaoni baada ya Tume ya kuajiri Walimu (TSC) kutangaza kwamba itahamisha huduma zake nyingi kwa mtandao.

Taarifa kutoka kwa afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia ilisema kwamba hapatakuwepo maombi ya moja kwa moja ya uajiri na upandishaji ngazi walimu kuanzia Machi Mosi.

Barua hiyo ni tarehe 15 Februari.

 

"Zoezi la kuanzisha matumizi ya barua pepe limeanza Februari 15 na litafungwa Aprili 30. Baada ya kumalizika kwa dirisha la usajili, barua pepe zote zilizo nje ya jukwaa la elektroniki hazitashughulikiwa," barua hiyo ilisema.

Jukwaa hili linalenga walimu wote walioajiriwa na Tume na wale wanaopitia programu za mafunzo.

Walimu wanaotafuta uhamisho sasa watawasilisha maombi yao mtandaoni na sio barua za moja kwa moja.

Huduma zingine ambazo zitapatikana kikamilifu mtandaoni ni maombi ya kupandishwa vyeo na usajili mpya wa walimu.

Maendeleo haya ya hivi punde yanajiri wakati TSC imekamilisha nyaraka za walimu za dijiti.

Kwa hivyo, maombi ya uhamisho yatapatikana kupitia tovuti ya Tume katika www.tsc.go.ke

Kwa kuongezea, Tume imeanzisha jukwaa la mtandaoni kwa barua pepe rasmi, mikutano na mafunzo mtandaoni.