Ibada ya wafu ya marehemu mbunge wa Juja yafanyika

Ibada wa wafu ya marehemu mbunge wa Juja Francis Munyua Waititu inafanyika leo Jumanne katika katika kanisa la chuo Kikuu cha JKUAT.

Rais Uhuru Kenyatta anaongoza viongozi wengine nchini katika ibada hiyo.

Marehemu alifariki siku ya Jumatatu wiki iliyopita baada ya kuugua saratani ya ubongo kwa muda mrefu.

Marehemu Waititu kwa jina la utani Wakapee alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Mp Shah Nairobi.

Familia yake ilisema imtaja kama mtu aliyependa amani na mabaye alikuwa tayari kutumikia wananchi. Familia ilisema kwamba siku ya mwisho alikuwa anahisi uchungu sana.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa miongoni mwa walioitakia familia hiyo salamu za rambi rambi. .

"Kwa masikitiko tumepoteza kiongozi aliyeenzi maendeleo, aliyeaminika na aliyejitolea kutokana na vitendo vyake vya wananchi aliowaongoza

Ni kwa sababu ya uaminifu na upendo ambao watu wa Juja walikuwa nao kwa Waititu ndio walimkabidhi muhula wa pili katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa licha ya ugonjwa wake," Rais alisema.

Kifo cha Wakapee kilijiri takriban siku saba baada ya kifo cha mbunge wa Bonchari John Oroo Oyioka.