Mbunge Sylvanus Osoro akamatwa na kuachiliwa kwa dhamana

Muhtasari

  • Alishtakiwa pia kwa kusababisha uharibifu wa mali wakati alipofika mbele ya Hakimu Mkuu wa Kisii Nathan Ashiundu.

  • Osoro alijisalimisha Jumatatu kwa Polisi wa Kisii Kati siku ya Jumatatu asubuhi baada ya siku moja akiwa mafichoni.

Mbunge wa Mugirango Kusini Sylivanus Osoro siku Jumatatu alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya uchochezi wa ghasia.

Alishtakiwa pia kwa kusababisha uharibifu wa mali wakati alipofika mbele ya Hakimu Mkuu wa Kisii Nathan Ashiundu.

Mbunge huyo hata hivyo aliachiliwa dhamana ya Shilingi laki moja na hakikisho lenye thamani sawa au dhamana ya pesa taslimu shilingi 50,000.

Alishtakiwa kwamba mnamo Machi 4, 2021 katika eneo la Kiomokama Kaunti Ndogo ya Masaba, huko Kisii, yeye, pamoja na wengine ambao hawakuwa kortini, kwa makusudi na kinyume cha sheria waliharibu gari kioo cha mbele, milango na madirisha vyenye thamani ya shilingi laki mbili mali ya Peter Karanja Njuguna.

Alikanusha mashtaka.

Mawakili wake Wilkins Ochoki na Alice Wahome walitaka dhamana kwa mbunge huyo.

Walieleza mahakama kuwa mbunge huyo hakuwa hawezi kukimbia na kwamba kurudi kortini kuhudhuria vikao vya kesi kila anapotakiwa kufanya hivyo.

Osoro alijisalimisha Jumatatu kwa Polisi wa Kisii Kati siku ya Jumatatu asubuhi baada ya siku moja akiwa mafichoni.

Mapema, katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kisii, wabunge Gladys Shollei na Mbunge wa Kandara Alice Wahome walipinga madai dhidi ya mbunge huyo.

"Tunachoona ni unyanyasaji wa korti na Serikali ambayo ni ya ukandamizaji," alisema Wahome.