Mutyambai awapandisha ngazi maafisa wakuu 20

Muhtasari

  • Wengi wa wale waliopandishwa ngazi wamekuwa katika ofisi zilizo na vyeo vya chini kwa hivyo kuathiri utendaji wao kwa amri.

  • Makamanda kadhaa wa mkoa pia walipandishwa cheo hadi manaibu wa Inspekta mkuu wa polisi (AIG) katika mabadiliko hayo.

Inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai
IG Hillary Mutyambai Inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai

Takriban maafisa wakuu wa polisi 20 wamepandishwa vyeo katika mabadiliko yaliyotangazwa na Inspekta Jenerali wa polisi Hilary Mutyambai.

Wengi wa wale waliopandishwa ngazi wamekuwa katika ofisi zilizo na vyeo vya chini kwa hivyo kuathiri utendaji wao kwa amri.

Tume ya Kitaifa ya Huduma za Polisi iliidhinisha kupandishwa cheo hadi kiwango cha Inspekta Mkuu Msaidizi Mwandamizi wa polisi(SAIG)kwa msaidizi mkuu wa IG Gideon Munga Nyale, naibu mkurugenzi wa Idara ya Kitaifa ya huduma za anga (NASD) Rodgers Mbithi, mkurugenzi wa Kitengo cha Mambo ya Ndani Mohamed Amin na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Nairobi Rashid Yakub.

 

Wengine waliopandishwa hadi cheo cha SAIG ​​ni pamoja na mkuu wa Chuo cha Kitengo cha Doria ya Mipaka huko Kanyonyo Abdulahi Aden, kamanda wa Polisi wa Reli Peter Ndung’u, mkuu wa mpiango katika kitengo cha AP na msemaji wa zamani wa polisi Masood Mwinyi na mkurugenzi wa wafanyikazi katika makao makuu ya polisi Boniface Maingi.

Makamanda kadhaa wa mkoa pia walipandishwa cheo hadi manaibu wa Inspekta mkuu wa polisi (AIG) katika mabadiliko hayo.

Wao ni pamoja na mkuu wa DCI Nairobi Bernard Nyakwaka, kamanda wa polisi wa mkoa wa Nyanza Karanja Muiruri, Augustine Nthumbi wa Kati na naibu mkurugenzi wa ofisi ya uchunguzi Carey Nyawinda.

Hatua ya Mutyambai inafuatia malalamishi ya baadhi yao kwamba walikuwa wamekaa kwenye vyeo vyao kwa muda mrefu.

Ili kuimarisha zaidi amri ya polisi mashinani, kambi zote za machifu, ambazo mwanzoni zilikuwa na AP, zimebadilishwa kuwa vituo vya polisi.

Kila kata katika nchi nzima sasa kina kituo cha polisi chini ya amri ya kamanda wa polisi wa wadi, ambaye alichukua nafasi ya OCS wa zamani.

Inspekta mkuu wa polisi alisema vituo hivyo ni sehemu kuu za utoaji wa huduma kwa umma.