Seneta Ochillo Ayacko ateuliwa kuongoza kamati ya uhasibu (CPAIC)

Muhtasari

• Ayacko anachukua nafasi ya seneta wa Kisii Sam Ongeri ambaye muda wake ulimalizika Disemba iliyopita.

• Kamati inasimamia matumizi ya mabilioni ya pesa za walipa ushuru zinazopewa serikali za kaunti chini ya hazina ya ugavi wa Mapato na ruzuku zingine za masharti.

Seneta wa Migori Ochillo Ayacko
Seneta wa Migori Ochillo Ayacko
Image: MAKTABA

Seneta wa Migori Ochillo Ayacko amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati yenye ushawishi ya seneti ya uangalizi inayosimamia mabilioni ya pesa zinazotengewa kaunti.

Atasaidiwa na seneta wa Marsabit Hargura Godaba ambaye alisalia katika wadhifa wa naibu mwenyekiti wa Kamati ya Uhasibu wa Umma na Uwekezaji (CPAIC).

Kamati hiyo, ambayo iliundwa upya simu ya Jumanne baada ya vuta ni kuvute miongoni mwa wanachama, ilifanya mkutano wake wa kwanza siku ya Alhamisi ambapo maseneta hao wawili waliteuliwa kama viongozi.

Ayacko anachukua nafasi ya seneta wa Kisii Sam Ongeri ambaye muda wake ulimalizika Disemba iliyopita.

Muda wa kamati iliyokuwa ikiongozwa na Ongeri uliisha Desemba iliyopita na ilibidi kamati hiyo iundwe upya kabla ya Bunge kuanza shughuli zake mwaka huu.

Ongeri alikuwa amechukuwa nafasi hiyo kutoka kwa seneta wa Homa Bay Moses Kajwang ’ambaye alikuwa ameshikilia nafasi hiyo kwa awamu tatu mfululizo.

Kamati inasimamia matumizi ya mabilioni ya pesa za walipa ushuru zinazopewa serikali za kaunti chini ya hazina ya ugavi wa Mapato na ruzuku zingine za masharti.

Jukumu lao ni sawa na la Kamati ya Uhasibu ya Umma (PAC) na Kamati ya Uwekezaji ya Umma (PIC) ya Bunge iliyopewa jukumu la kukagua matumizi ya serikali za kitaifa.

Maseneta wamekuwa waking’ang’ania nafasi katika kamati hiyo ya wanachama tisa kuhusu kile wanasema ni ‘kutambulika’ kutokana na ushawishi wa kamati hiyo.

Wanachama wa Kamati hiyo ni pamoja na Imana Malachy Ekal (Turkana), Njeru Ndwiga (Embu), Christopher Lang'at (Bomet) na Mercy Chebeni (seneta maalum) Wengine ni Fatuma Dullo (Isiolo), Kimani Wamatangi (Kiambu) na Johnes Mwaruma (Taita Taveta).

Wamatangi alirejea kwa kamati hiyo baada ya kuchukuwa nafasi mwenzake wa Muranga Irungu Kang’ata kama kiranja wa wengi.