Wanaharakati walalamikia ufisadi katika kaunti ya Bungoma

Muhtasari

• Ripoti ya mkaguzi wa mkaguzi wa matumizi ya pesa za umma iliitaja kaunti ya Bungoma miongoni mwa Kaunti zilizotumia vibaya mgao wa pesa za kukabili janga la Covid-19.

Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati
Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati
Image: JOHN NALIANYA

TAARIFA YA JOHN NALIANYA

 

Wanaharakati wa kisiasa Kaunti ya Bungoma chini ya vuguvugu la Bungoma Liberation  wanamtaka Gavana wa Kaunti hiyo Wycliffe Wangamati kujitokeza wazi kuelezea jinsi serikali ya Kaunti hiyo ilivyotumia mgao wa fedha za kukabili msambao wa virusi vya Korona.

Kwenye taarifa kwa wanahabari mwishini mwa wiki, Isaiah Sakonyi ambaye ni msemaji wa vuguvugu hilo, alikosoa serikali ya Kaunti kuhusu madai ya kuongezeka kwa visa vya   ufisadi katika kaunti hiyo.

Ripoti ya mkaguzi wa mkaguzi wa matumizi ya pesa za umma iliitaja kaunti ya Bungoma miongoni mwa Kaunti zilizotumia vibaya mgao wa pesa za kukabili janga la Covid-19.

Wakati huo huo, wanaharakati hao wameilaumu serikali ya Kaunti kwa kuwahangaisha wapinzani wake ikiwemo kuwatia mbaroni bila sababu za kimsingi.