Covid - 19; Kenya yatakiwa kuruhusu hospitali za kibinafsi kuagiza chanjo

Muhtasari

• Kenya ilipiga marufuku uingizaji wa kibinafsi wa chanjo ya Covid-19 mnamo Aprili 2 baada ya kampuni moja kuleta Sputnik V, ambayo haina leseni ya matumizi ya dharura kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni.

Rais Uhuru Kenyatta akipokea chanjo ya Covid-19
Rais Uhuru Kenyatta akipokea chanjo ya Covid-19

TAARIFA YA JOHN MUCHANGI 

Shirika la Afrika CDC limeiomba Wizara ya Afya kuruhusu sekta ya binafsi kuagiza chanjo za Covid-19.

Kenya ilipiga marufuku uingizaji wa kibinafsi wa chanjo ya Covid-19 mnamo Aprili 2 baada ya kampuni moja kuleta Sputnik V, ambayo haina leseni ya matumizi ya dharura kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni.

Naibu mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Afrika Dr Ahmed Ogwell alisema sekta ya binafsi inaweza chanja angalau asilimia 30 ya Wakenya ifikapo mwisho wa mwaka ujao.

 

Walakini, alisema wanahitaji kuagiza chanjo kupitia mfumo sahihi uliowekwa na Wizara ya Afya.

Kulingana na mkuu wa kikosi kazi cha utoaji chanjo, Dk Willis Akhwale, Kenya imerekebisha mpango wake wa chanjo na inakusudia kufikia asilimia 60 ya idadi ya watu ifikapo mwisho wa mwaka ujao.

Ogwell, mtaalam wa afya ya umma wa Kenya aliyeko mjini Addis Ababa, alizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na wafanyibiashara katika sekta ya Afya barani Afrika (Africa Health Business ) siku ya Jumanne.

"Tunahitaji mifumo mizuri iliyoundwa na serikali kwa hivyo ni muhimu kumchunguza ambaye anaagiza chanjo kutoka nje. Kuwa na pesa nyingi sio vigezo vya nani wa kwanza kwenye foleni ya kuingizwa. Ni muhimu kwamba ni sekta ya binafsi ya kweli pekee inayopata leseni ya chanjo, lakini kupitia utaratibu wa serikali uliowekwa vizuri, ”alisema.

"Chanjo zinazonunuliwa nje ya njia hizi ni hatari kwa sababu zinaweza kufungua nafasi ya bidhaa za ghushi."

 

Kenya imewachanja watu wapatao milioni moja lakini inalenga watu wasiopungua milioni 25 ifikapo mwisho wa mwaka ujao kufikia kinga ya kamili.

Ogwell alisema kufikia Mei 18, Afrika nzima ilikuwa imeingiza dozi milioni 38 za aina tofauti za chanjo za Covid. Kati ya hizi 38, dozi milioni 22 tu ndizo zimetumika.

“Hii inatuambia kuwa tuko mkiani mwa kupokea chanjo. Sisi ni watu bilioni 1.3, kwa hivyo tuko mbali na lengo milioni 738. Hata kidogo tunayopokea hatupati chanjo na hii inakuambia mchakato ni polepole. Sio chanjo zinazookoa maisha, kinachookoa maisha ni kuchanjwa, "alisema.

Alisema utaratibu wa Covax ambao Kenya inategemea unaweza tu kufikia asilimia 30 ya idadi ya watu mwishoni mwa mwaka ujao. Alisema asilimia 30 iliyobaki inaweza kufunikwa tu na ushiriki wa sekta binafsi.

Ogwell alisema vituo vya kibinafsi vinaweza kuagiza kupitia shirika la Upataji Chanjo la Afrika la  AU, (Avatt) mara tu serikali itakaporuhusu.

"Avatt haijaamriwa kuuza moja kwa moja kwa sekta  za binafsi, lakini tutarahisisha sekta ya binafsi kununua chanjo ili tufikie asilimia 60," alisema.