Polisi wanaohusishwa na mauaji ya ndugu wawili kutoka Kianjokoma waachiliwa kwa dhamana

Wameagizwa walipe bondi ya milioni tatu ama dhamana ya pesa taslimu Sh300,000.

Muhtasari

• Jaji Daniel Ogembo hata hivyo amewazuia sita hao dhidi ya kuenda katika eneo la Kianjokoma ambapo mauaji hayo yalitokea.

Polisi sita ambao walishtakiwa kwa mauaji ya ndugu wawili Embu wakiwa mahakamani
Polisi sita ambao walishtakiwa kwa mauaji ya ndugu wawili Embu wakiwa mahakamani
Image: MAKTABA

Habari na Annette Wambulwa

Maafisa sita wanaohusishwa na mauaji ya ndugu wawili katika eneo la Kianjokoma, kaunti ya Embu wameachiliwa kwa dhamana.

Sita hao; Benson Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruiyot, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwaniki wameagizwa walipe bondi ya milioni tatu ama dhamana ya pesa taslimu Sh300,000.

Hali kadhalika jaji Daniel Ogembo hata hivyo amewazuia sita hao dhidi ya kuenda katika eneo la Kianjokoma ambapo mauaji hayo yalitokea.

Hata hivyo mmoja wa washukiwa, Mputhia ambaye nyumbani kwake ni Meru ameruhusiwa kupitia Embu akielekea nyumbani .

Mnamo mwezi Septemba sita hao walikanusha mashtaka ya mauaji dhidi ya yao.

Upande wa mashtaka uliomba washukiwa wa kiume wazuiliwe katika gereza ya Industrial Area huku wale wa kiume wakizuiliwa katika gereza ya wanawake ya Lang'ata.