Covid-19:Watu 53 wapatikana na corona,17 wapona, 2 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,781 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.1%
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 19 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 95
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,807,014
Image: HISANI

Kenya imesajili visa 53 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 5,031 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 48 ni wakenya huku 5 wakiwa raia wa kigeni,32 ni wanaume huku 21 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,781 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.1%.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 19 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 95.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,807,014.

Aidha watu 17 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,992,12 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 5 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Watu 2 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,330.

Kuna wagonjwa 348 ambao wamelazwa hospitalini, 975 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 20 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,494,091