Maelfu wajitokeza kwa mkutano wa azimio la umoja

Muhtasari

• Mbunge wa Suna kusini Junet Mohammed amewakishishia wananchi kuwa mipango yote imekamilika kwa hafla ya leo.

Ruth Mumbai (kushoto), Grace Kamau na Jane Waithera katika mkutano wa Azimio la Umoja Desemba 10, 2021. Picha/ Fredrick Omondi
Ruth Mumbai (kushoto), Grace Kamau na Jane Waithera katika mkutano wa Azimio la Umoja Desemba 10, 2021. Picha/ Fredrick Omondi

Siku ya wafuasi wa ‘Baba’ kubaini  njia watakayofuata  ifikiakapo siku ya uchaguzi.

Macho yote  ni katika uwanja wa michezo wa Kasarani ambapo kinara wa ODM Raila Odinga anatarajiwa kutangaza azma ya kugombea urais mwaka ujao.

 Njia zotezinaelekea Kasarani ambapo viongozi kutoka maeneo yote nchini wanaonekana kupata mwaliko rasmi.

 Mbunge wa Suna kusini Junet Mohammed amewakishishia wananchi kuwa mipango yote imekamilika kwa hafla ya leo.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho amewaomba wakenya hasa wale ambao wametoka Mombasa  wasikize kitakacho jadiliwa  Kasarani.

Inatarajia kuwa Raila atawasili uwanja wa Kasarani mwendo wa saa 11:30 ambapo viongozi wa vyama ambavyo vinapigia upato waziri mkuu kufika ikulu watamkaribisha. Inasemekana kiongozi huyo atatangaza ikiwa azma yake ya urais katika uchaguzi wa 2022

Vigogo wa siasa, Musalia Mudavadi   kinara wa ANC , Kalonzo Musyoka wa wiper na Moses Wetang’ula wa Ford Kenya wamesema hawataweza kufika kwa mkutano huo kwa sababu wao pia walikuwa na mikutano mingine ya kujipigia debe.

Uwanja wa kasarani ulifunguliwa mwendo wa saa 6:30 ambapo wananchi walianza kuingia na kujichukulia viti kungoja kuhutubiwa

Zaidi ya magava 30 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo na mamia ya wabunge.