Je, OKA itaweza kushtahimili joto la kisiasa hadi uchaguzi ujao kama vinara wake wanavyosema?

Muhtasari

•Musalia akizungumza wakati wa mazishi ya Mama Rosebella Jerono alisema malengo yao kama muungano ni kuhakikisha wanatoa mgombeaji wa kiti cha urais.

•Vinara hao isipokuwa Gideon Moi walikosa kudhuria mkutano wa uzinduzi wa vuguvugu la Azimio La Umoja ambapo kila kinara alitoa sabau za kutohudhuria.

Viongozi wa OKA Moses Wetang'ula, Kalonzo Musyoka na Gideon Moi wakati wa ibada ya kumuaga Mama Rosebella Jerono Mudavadi katika Kanisa la Friends Church-Quakers mnamo Desemba 16.
Viongozi wa OKA Moses Wetang'ula, Kalonzo Musyoka na Gideon Moi wakati wa ibada ya kumuaga Mama Rosebella Jerono Mudavadi katika Kanisa la Friends Church-Quakers mnamo Desemba 16.
Image: MERCY MUMO

Vinara wa muungano wa OKA Jumatano walijitokeza na kutangaza wazi kwamba watashikamana na kuhakikisha wametoa mgombeaji wa kiti cha urais.

Vinara wa muungano huo ni pamoja na Kalonzo Musyoka wa Wiper, Moses Wetang’ula wa Fork-k, Gideon Moi wa KANU na Musalia Mudavadi wa ANC.

Musalia akizungumza wakati wa mazishi ya Mama Rosebella Jerono alisema malengo yao kama muungano ni kuhakikisha wanatoa mgombeaji wa kiti cha urais.

Ikikumbukwe vinara hao isipokuwa Gideon Moi walikosa kudhuria mkutano wa uzinduzi wa vuguvugu la Azimio La Umoja ambapo kila kinara alitoa sabau za kutohudhuria.

Siku ya Jumatano Naibu rais William Ruto akiwa kwenye mkutano na wakazi wa Lugari aliwahimiza kinara wa ANC Musalia Mudavadi na kinara wa Ford kenya Moses Wetangula wajiunge naye akiwaahidi kupata mgao mkubwa katika serikali yake.

Aliwauliza waliohudhuria kama wangetaka wafanye kazi pamoja na viongozi hao na kwa pamoja wakakubali.

“Nyinyi ni watu wa kupangwa? mnataka tufanye kazi na Mudavadi na Wetang’ula “ Umati kwa pamoja ulikubali Ruto kufanya kazi pamoja na vinara hao wa OKA.

Swali lililosalia kwa wengi ni kweli mungaano huu utasimamisha mgombezi wa urais 2022?