Polisi kumhoji Dennis Itumbi kuhusu utekaji nyara na kuteswa kwake

Muhtasari

•Timu inayofuatilia kesi hiyo imesema wanasubiri Itumbi apate nafuu hospitalini na ili waweze kuzungumza naye na kuchukua taarifa yake.

•Msemaji wa polisi Bruno Shioso alisema wanachunguza kubaini sababu na waliohusika na tukio hilo.

•Itumbi amekuwa mwiba kwa viongozi wakuu serikalini, ambao baadhi yao amewataja kuwa wezi wa ardhi

Image: TWITTER// DAVID ITUMBI

Wapelelezi wanapanga kumhoji mwanablogu Dennis Itumbi na ambaye pia ni mtaalamu wa mikakati ya kidijitali wa Naibu Rais William Ruto kuhusiana na madai kuwa alitekwa nyara na kunyanyaswa.

Timu inayofuatilia kesi hiyo imesema wanasubiri Itumbi apate nafuu hospitalini na ili waweze kuzungumza naye na kuchukua taarifa yake.

Timu hiyo pia itazungumza na walioshuhudia kisa hicho kikitendeka nje ya duka moja la kinyozi katika eneo la Thindigwa, kaunti ya Kiambu, mnamo mkesha wa Krismasi.

Mahojiano haya yatawapa picha wazi ya nini hasa kilifanyika.

Timu inayoendeleza uchunguzi bado haijatembelea eneo la tukio.

Walisema juhudi zao za kulitafuta gari linalosemekana kutumika katika utekaji nyara huo hazikufua dafu.

Polisi wanasema maelezo ya gari lililotolewa na mashahidi hayalingani na rekodi rasmi.

"Itakuwa muhimu kusikia kutoka kwake (Itumbi), sio marafiki zake au wanasiasa. Tutasubiri wakati huo kwa sababu mengi yatatolewa katika mwelekeo wa uchunguzi na nia, "afisa mkuu anayefahamu uchunguzi huo alisema.

Itumbi amekuwa mwiba kwa viongozi wakuu serikalini, ambao baadhi yao amewataja kuwa wezi wa ardhi. Amekuwa akimwita askari polisi mkuu "kikaragosi" na kuwatambulisha walengwa wake kwenye mitandao ya kijamii.

Msemaji wa polisi Bruno Shioso alisema wanachunguza kubaini sababu na waliohusika na tukio hilo.

"Tunatoa wito kwa umma kuwa na subira wakati wa uchunguzi na hivyo wanapaswa kuacha uvumi," Shioso. sema.

“Pia tunatoa wito kwa wananchi ambao wanaweza kuwa na taarifa za tukio hilo kujitolea na kuripoti katika kituo chochote cha polisi au kupitia nambari yetu ya simu 999,112 au 0800 722203,” alisema

Itumbi bado yuko hospitalini akiugiza majeraha baada kutekwa nyara kwa njia ya tatanishi. Waliomtembelea Jumamosi walisema anazungumza kwa roho ya ucheshi na hayumo hatarini.

Alitekwa nyara mnamo Alhamisi na kupigwa kabla ya kutelekezwa kando ya barabara akiwa uchi katika eneo la Lucky Summer, Kasarani.

Alikuwa na majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wakati alipatikana na dereva wa teksi. Alipelekwa hospitalini Ijumaa asubuhi.

(Utafsiri: Samuel Maina)