Baba atosheleza kiu chake cha mapenzi na mwanawe baada ya kumwandalia chajio cha kifahari Makueni

Jamaa huyo alimwandalia mwanawe chakula kizuri cha jioni kabla ya kumwalika kitandani chake

Muhtasari

•Benjamin Kavindu  35, alikamatwa Jumanne baada ya mwanawe wa darasa la saba kuripoti kuhusu unyama aliomtendea wakati mama hakuwepo nyumbani.

•Baada ya kutosheka Kavindu aliamurisha mwanawe aoge mara moja na kumuonya dhidi ya kuambia yeyote kuhusu kilichotokea.

Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi katika kaunti ya Makueni wanazuilia jamaa mmoja anayeripotiwa kujitosheleza kimapenzi na mwanawe wa kambo mwenye umri wa miaka 12 usiku wa Jumapili katika eneo la Kibwezi.

Benjamin Kavindu Mwania 35, alikamatwa Jumanne baada ya mwanawe ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba kuripoti kuhusu unyama aliomtendea wakati mama hakuwepo nyumbani.

Mtoto huyo alisimulia polisi katika kituo cha Ulilinzi kuhusu jinsi babake alivyomwandalia chakula kizuri cha jioni kabla ya kumwalika kwenye kitanda chake.

Kitengo cha DCI kimeripoti kwamba baada ya mtoto huyo kukubali ombi la babake la kuandamana naye kitandani alimgeukia na kukata kiu chake cha ngono, kinyume na matarajio yake.

Baada ya kutosheka Kavindu aliamurisha mwanawe aoge mara moja na kumuonya dhidi ya kuambia yeyote kuhusu kilichotokea.

Mtoto huyo hata hivyo aliamua kufungukia mamake ambaye hakuwepo usiku wa tukio kisha wakaandamana hadi kituo cha polisi na kupiga ripoti.

Msako ulianzishwa mara moja na mshukiwa akanaswa akiwa katika eneo la Miangeni na kutiwa pingu.

Mhasiriwa alipelekwa katika hospitali moja ya Kibwezi ambako alihudumiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Kavindu anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ambayo yatapendekezwa na maafisa wa usalama.