Mimi ndiye chaguo bora kwa wakenya - Jimmy Wanjigi

Muhtasari

• Mfanyibiashara maarufu nchini Jimmy Wanjigi ameendelea kujipigia debe kwa kile anachokitaja kuwa yeye ndo mtu wa pekee anayeweza kuiongoza nchi hii kuafikia malengo yake ya kimaendeleo.

• Wanjigi amekiri kwamba atakuwa anawania kiti hicho cha urais kupitia tikiti ya chama cha ODM huku ikisubiriwa kuona iwapo atambwaga Raila Odinga katika kura za mchujo za chama hicho.

Image: Hisani

Mfanyibiashara maarufu nchini Jimmy Wanjigi ameendelea kujipigia debe kwa kile anachokitaja kuwa yeye ndo mtu wa pekee anayeweza kuiongoza nchi hii kuafikia malengo yake ya kimaendeleo.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini, Wanjigi amewakosoa wakenya wanaodinda kupiga kura akisema kwamba wanasiasa huchangia pakubwa hali ya maisha na uchumi kwa ujumla.

Aidha amesema kwamba alichangia pakubwa katika ujenzi wa barabara kuu ya Thika na pia kuchangia katika mchakato wa kuwaunganisha baadhi ya wanasiasa, akiamini kwamba hayo ni baadhi ya mambo anayoweza kuyatumia kuboresha hali ya taifa hili.

Wanjigi amekiri kwamba atakuwa anawania kiti hicho cha urais kupitia tikiti ya chama cha ODM huku ikisubiriwa kuona iwapo atambwaga Raila Odinga katika kura za mchujo za chama hicho.

Ameongeza kwamba kuna baadhi ya viongozi ambao wameendeleza ukoloni mamboleo kwa kutumia nafasi zao vibaya kuwakandamiza wakenye na kuzidi kujitajirisha.

Amepinga mswada wa BBI akisema kwamba haukulenga kupigania wananchi bali kubuni nafasi kwa viongozi wachache, akisema kwamba wakenya hawakuhusishwa katika kutoa maoni yao kuhusu mswada huo.

Vilevile amejitenga na mpango wa chama cha UDA akisema kwamba maono yao ni tofauti na hadhani watafanya kazi pamoja kwa sasa.