Kivutha Kibwana atoa sababu 10 kuu za kumuunga Raila odinga

Muhtasari
  • Kivutha Kibwana atoa sababu 10 kuu za kumuunga Raila odinga
Charity Ngilu wa NARC, Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna na Prof. Kivutha Kibwana wa chama cha Muungano wakati wa kongamano la NARC NDC katika ukumbi waBOMAS
Image: Fredrick Omondi

Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana ameorodhesha sababu 10 za kuunga mkono urais wa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

Kibwana alikuwa akizungumza Ijumaa katika ukumbi wa Bomas  wakati wa Kongamano la Wajumbe wa Kitaifa wa vyama vya Narc na Muungano.

Hizi ndizo sababu;

  1. Mkombozi wa pili 
  2. Kukomaa/Kufikia hatua ya kujitambua 
  3. Mjenzi wa makubaliano 
  4. Bingwa wa ugatuzi 
  5. Mtetezi wa Katiba 
  6. Kiongozi wa dunia anayetambulika
  7. Umetekeleza kazi halisi katika nyadhifa zote za serikali ulizoshika
  8.  Anaelewa shughuli za serikali na takriban viongozi wote
  9. Mtetezi wa wanyonge
  10. Mpiganaji wa watu na Mpiganaji wa ufisadi

Raila alifika Bomas of Kenya kupamba Kongamano la pamoja la Wajumbe wa Kitaifa kwa vyama vya Muungano na Narc.

Ngilu na Kibwana walisema kuwa vyama vyao havitasimamisha wagombea urais katika uchaguzi ujao

Badala yake, vyama vya Narc na Muungano vitamuunga mkono Raila chini ya muungano wa Azimio la Umoja Movement.