Rais Kenyatta akutana na viongozi wa Mt Kenya

Muhtasari

• Mkutano huo wa siku ya Jumatano uliofanyika katika Ikulu ndogo ya Sagana katika Kaunti ya Nyeri ulileta pamoja Magavana wa eneo hilo, Wabunge na Wakilishi wa wadi.

• Lengo hasa la mkutano huo ni kudumisha umoja huku taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.

• Uhuru alitumia fursa hiyo kuwafafanulia wakaazi ajenda ya serikali kuhusu miradi mbalimbali katika eneo hilo na sehemu zingine nchini.

Rais Uhuru Kenyatta ahutubia viongozi wa Mlima Kenya katika Ikulu ndogo ya Sagana, 2/23/2022
Rais Uhuru Kenyatta ahutubia viongozi wa Mlima Kenya katika Ikulu ndogo ya Sagana, 2/23/2022
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na viongozi wa tabaka mbali mbali kutoka eneo la Mlima Kenya ikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi.

Mkutano huo wa siku ya Jumatano uliofanyika katika Ikulu ndogo ya Sagana katika Kaunti ya Nyeri ulileta pamoja Magavana wa eneo hilo, Wabunge na Wakilishi wa wadi.

Kulingana na taarifa ya Ikulu lengo hasa la mkutano huo ni kudumisha umoja huku taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.

Wakati huo huo, Kiongozi wa Taifa atatumia fursa hiyo kuwafafanulia wakaazi ajenda ya serikali kuhusu miradi mbalimbali katika eneo hilo na sehemu zingine nchini sawa na mstakabali wa miradi hiyo baada ya uchaguzi.

Alipowasili saa sita unusu kwenye mkutano huo, Rais Kenyatta alilakiwa na Mawaziri Mutahi Kagwe, Peter Munya, James Macharia na Prof Margaret Kobia miongoni mwa maafisa wengine wakuu serikalini.