Pesa zangu zote nimezipata kihalali - Evans Kidero

Muhtasari

• Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi, Evans Kidero amesema kwamba mali yake yote ni halali na kwamba anaweza kuthibitisha kuhusu hilo,kauli hii ikijiri wakati anazidi kuchunguzwa na mamlaka ya kulipa kodi nchi KRA kuhusu pesa alizozitumia katika uchaguzi mkuu uliopita.

• Mwanzoni mwa mwezi huu KRA ilimtaka Kidero kulipa shilingi 427,269,795, kama kodi ya pesa zote alizotumia katika kampeni zake.

 

KIDERO-1
KIDERO-1

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi, Evans Kidero amesema kwamba mali yake yote ni halali na kwamba anaweza kuthibitisha kuhusu hilo,kauli hii ikijiri wakati anazidi kuchunguzwa na mamlaka ya kulipa kodi nchi KRA kuhusu pesa alizozitumia katika uchaguzi mkuu uliopita.

Kidero anashtumiwa kwa kutumia hela nyingi katika kamapeni zake za  kuwania kiti cha ugavana kaunti ya Nairobi ila akakwepa kulipa kodi .

“Kabisa, ninaweza kuthibitisha, ndo maana nilishinda kesi katika mahakama ya KRA,” Kidero alisema.

Mwanzoni mwa mwezi huu KRA ilimtaka Kidero kulipa shilingi 427,269,795, kama kodi ya pesa zote alizotumia katika kampeni zake.

Katika uamuzi wa 4/2/2022. Jaji David Majanja alisema kwamba Kidero alikosa kuthibitisha kwamba pesa hizo zilikuwa zimetengewa kampeni na kwamba kwa hakika zilitumika kutekeleza jukumu hilo.

​​Amri hiyo ilitokana na ripoti ya uchunguzi iliyowasilishwa na KRA kuhusu jinsi pesa hizo zilivyopatikana na kutumika.

“Mahakama hii inakubaliana na kamishna wa KRA kwamba haijulikani mshatikwa alipata pesa hizo kwa njia gani, na hivyo basi anahitajika kulipa shilingi 423,000,000 kama kodi ya pesa zote alizozitumia katika kampeni,” Majanja alisema.

Kidero tayari ameshatangaza azma yake ya kuwania kiti cha ugavana katika kaunti ya Homabay.