Gavana wa zamani wa Nairobi Evans Kidero apatikana na corona

Muhtasari
  • Aliyekuwa gavana wa Nairobi Evans Kidero, kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook ametangaza kwamba amepatikana na virusi vya corona, siku chache baada ya kupokea chanjo ya corona
  • Kidero alipimwa siku ya Jumanne Aprili,6 pamoja na familia yake ambao hawajapatikana na virusi hivyo, alisema Kidero
evans-kidero
evans-kidero

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Evans Kidero, kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook ametangaza kwamba amepatikana na virusi vya corona, siku chache baada ya kupokea chanjo ya corona.

Kidero alipimwa siku ya Jumanne Aprili,6 pamoja na familia yake ambao hawajapatikana na virusi hivyo, alisema Kidero.

Pia alisema kwamba dalili a maradhi hayo zilianza wiki moja baada ya kupokea chanjo dhidi ya virusi vya corona.

 

"Wapendwa wakenya, nilipokea chanjo ya virusi vya corona tarehe 29/03/2021, ambapo ilifuatiwa na dalili za maradhi hayo siku tatu baadaye

kama familia tulipimwa corona jana, JUmanne, ambapo nimepokea ripoti, kila mtu hana virusi hivyo isipokuwa mimi

Nitaanza kujitenga kwa wiki mbili," Alisema Kidero.

Mwanasiasa huyo amewahimiza wale wote ambao ametangamana nao kwa siku zilizopita waweze kuenda kupimwa.

"Nawashauri wanakamati wettu ambao nimetangamana nao waende wakapimwe corona kwa upesi, pia nawahimiza wakenya wote wazidi kuata na kutii kanuni za wizara ya afya, valia barakoa, osha mikono yako kwa sabuni na maji masafi 

Tumia vieuzi na mpate chanjo ya corona,"