Katombi hatimaye wazimwa baada ya kuhangaisha wakazi wa Nairobi

Muhtasari

•Kababa ambaye alifanywa kiongozi wa genge hilo sugu kufuatia kifo cha Mgaza alifariki usiku wa Jumanne katika tukio la risasi baada ya kukaidi amri ya kujisalimisha.

•Kababa ambaye alifanywa kiongozi wa genge hilo sugu kufuatia kifo cha Mgaza alifariki usiku wa Jumanne katika tukio la risasi baada ya kukaidi amri ya kujisalimisha.

•Wakati milio ya risasi iliisha, mwili wa Kababa ulikuwa umelala chini huku mwenzake ambaye ndiye apekee aliyesalia akifanikiwa kutoroka na majeraha.

Crime Scene

Takriban wiki mbili baada ya kiongozi wa Katombi Fadhili Mgaza kuuawa, genge hilo limepata pigo zaidi baada ya polisi kufanikiwa kumuangamiza mridhi wake Jakande Kabede almaarufu Kababa.

Kababa ambaye alifanywa kiongozi wa genge hilo sugu kufuatia kifo cha Mgaza alifariki usiku wa Jumanne katika tukio la risasi baada ya kukaidi amri ya kujisalimisha.

Kulingana na DCI, genge hilo ambalo limekuwa likihangaisha wakazi wa mitaa ya Pangani, Huruma na Mathare lilikuwa limebadilisha jina na kujiita'Yeyoye' katika juhudi za kujificha polisi baada ya kiongozi wao kuuawa siku kadhaa zilizopita.

Usiku wa Jumanne Kababa na mwenzake mmoja walishambulia mtaa wa Mathare na kuwapora wakazi waliokuwa wanaelekea nyumbani kabla ya polisi kutoka kituo cha Pangani kufikishiwa habari.

Baada ya polisi kufahamishwa kuhusu uhalifu uliokuwa unaendelea walikimbia katika eneo la tukio na kupata majambazi hao wawili wakipora mkoba wa mwanamke.

Koplo ambaye alikuwa anaongoza operesheni hiyo aliamrisha wawili hao wajisalimishe ila mmoja wao akapiga risasi na ambayo ilikosa bega la afisa huyo kwa inchi kidogo tu.

Kufuatia hayo milio ya risasi ilitanda hewani huku maafisa wakijibu mashambulizi ya majambazi hao. Wakati milio ya risasi iliisha, mwili wa Kababa ulikuwa umelala chini huku mwenzake ambaye ndiye apekee aliyesalia akifanikiwa kutoroka na majeraha.

Marehemu alipatikana na bastola mpja na risasi nne kabla ya mwili wake kupelekwa mochari. Wakenya wamehimizwa kuendelea kushirikiana na polisi katika juhudi zao za kuzima magenge ya wahalifu nchini.