Taarifa ya bajeti kuwasilishwa bungeni Aprili 7 - Waziri Yatani

Muhtasari
  • Uwasilishaji wa taarifa ya bajeti unatarajiwa kuwa wa mwisho kwa Yatani chini ya utawala uliopo
Waziri Ukur Yatani
Image: Fredrick Omondi

Taarifa ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022/2023 itawasilishwa tarehe 7 Aprili, 2022 kuanzia saa tisa jioni.

Waziri wa Hazina Ukur Yatani alitangaza hayo Jumatatu.Bajeti hiyo itawasilishwa kwenye bunge la kitaifa.

Uwasilishaji wa taarifa ya bajeti unatarajiwa kuwa wa mwisho kwa Yatani chini ya utawala uliopo.

Bajeti itasomwa miezi miwili mapema mwaka huu katika uchaguzi wa Agosti 9.