Dozi 840,000 za chanjo ya Astrazeneca zimeharibika - MoH

Muhtasari

• Wizara ya afya Jumatano ilitangaza kwamba dozi 840,000 za chanjo ya Astrazeneca zimeharibika baada ya muda wake wa matumizi kukamilika.

• Viwango vikubwa vya chanjo zilizoharibika vimeripotiwa katika kaunti za Nakuru [35,000], Busia [27,956], Kajiado [25,770], Kakamega [12,000] na Kwale [11,730].

MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS

Wizara ya afya Jumatano ilitangaza kwamba dozi 840,000 za chanjo ya Astrazeneca zimeharibika baada ya muda wake wa matumizi kukamilika.

 Aidha, inakisiwa kwamba huenda dozi zingine milioni moja za chanjo ya Johnson and Johnson zitaharibika iwapo hazitatumika ifikiapo 15/4/2022.

Viwango vikubwa vya chanjo zilizoharibika vimeripotiwa katika kaunti za Nakuru [35,000], Busia [27,956], Kajiado [25,770], Kakamega [12,000] na Kwale [11,730].

Kulingana na ripoti ya wizara ya afya, tarehe ya mwisho ya matumizi ya chanjo hizo ilikuwa 28/2/2022.

Hali hii inajiri kwa kile kinasemekana kuwa wananchi wengi kutojitokeza kupata chanjo ili kujikinga na janaga la Corona.

Ifahamike kwamba waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kwamba serikali haitamlazimisha mkenya yeyote kupata chanjo, na kwamba itakuwa kwa hiari.