MAADHIMISHO

Rais Ruto awasili Uganda

Rais Ruto atajiunga na nchi hiyo kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru.

Muhtasari

•Waliondamana naye ni pamoja na Mke wa Rais Rachael Ruto na ujumbe wa hadhi ya juu wa viongozi wa Kenya akiwemo waziri mteule wa Baraza la Mawaziri la Masuala ya Kigeni Alfred Mutua.

•Safari ya Ruto nchini Uganda inajiri siku chache baada ya mwanawe Museveni, Muhoozi Kainerugaba, kuzua taharuki ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili jirani kufuatia machapisho yake tatanishi kwenye mitandao ya kijamii.

Image: RACHEL RUTO/TWITTER

Rais wa Kenya William Ruto amewasili nchini Uganda kuhudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa nchi hiyo mnamo Jumapili.

Waliondamana naye ni pamoja na Mke wa Rais Rachael Ruto na ujumbe wa hadhi ya juu wa viongozi wa Kenya akiwemo waziri mteule wa Baraza la Mawaziri la Masuala ya Kigeni Alfred Mutua.

Safari ya Ruto nchini Uganda inajiri siku chache baada ya mwanawe Museveni, Muhoozi Kainerugaba, kuzua taharuki ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili jirani kufuatia machapisho yake tatanishi kwenye mitandao ya kijamii.

Muhoozi alikuwa amedai kuwa angeteka Nairobi baada ya wiki mbili. Kauli yake ilizua hisia mchanganyiko kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya na Uganda na kumlazimu Museveni kuomba msamaha.

Siku kadhaa baadaye, Museveni alisema kuwa haikuwa sahihi kwa mwanawe kutoa matamshi kama hayo.

"Nasikitika sana kwa kitendo alichofanya mwanangu Muhoozi. Naomba ndugu zetu wa Kenya watusamehe kwa ujumbe wa Twitter uliotumwa na Jenerali Muhoozi, aliyekuwa Kamanda wa Majeshi ya Nchi Kavu," Museveni alisema.