Sakaja akutana na maafisa wa KMPDU ili kuzuia mgomo wa madaktari

Madaktari hao wamelaumu kaunti kwa kukosa kutekeleza Mkataba wao wa Makubaliano ya Pamoja (CBA) wa 2017-2021

Muhtasari
  • Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini (KMPDU) ulitoa notisi ya mgomo ili hatua ya kiviwanda ianze Januari 6, 2023 katika kaunti zote
Sakaja akutana na maafisa wa KMPDU ili kuzuia mgomo wa madaktari
Image: JOHNSON SAKAJA/TWITTER

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amewasiliana na muungano wa madaktari katika jitihada za kuepusha mgomo wa madaktari unaokaribia mwezi Januari.

Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini (KMPDU) ulitoa notisi ya mgomo ili hatua ya kiviwanda ianze Januari 6, 2023 katika kaunti zote.

"Mwenyekiti wa Afya wa COG @MuthomiNjuki leo tumekutana na Uongozi wa Kitaifa wa @kmpdu kutatua masuala ambayo yamesababisha wahudumu wa afya kutoa notisi ya mgomo wa kitaifa kwa tarehe 6 mwezi huu. January. Tunafanya maendeleo makubwa na nina imani kwamba tutaepusha mgomo huu," Sakaja alisema.

Madaktari hao wamelaumu kaunti kwa kukosa kutekeleza Mkataba wao wa Makubaliano ya Pamoja (CBA) wa 2017-2021 ambao walitia saini Machi 2017 baada ya mgomo kulemaza wa siku 100.

Wanashutumu Wizara ya Afya, serikali za kaunti na mashirika ya umma kwa kutelekeza utekelezaji wa CBA na urekebishaji wa mishahara yao, na kukosa kutuma wahudumu wa matibabu miongoni mwa maswala mengine.

"Zaidi ya wanafunzi 1000 wamekaa nyumbani kwa zaidi ya mwaka mmoja wakisubiri kutumwa na kuajiriwa," katibu mkuu wa KMPDU Davji Atellah alisema katika taarifa yake Desemba 20.