MCA wa Korogocho afikishwa mbele ya mahakama Nairobi

Polisi wanasema kwamba wanahitaji siku saba zaidi kukamilisha uchunguzi.

Muhtasari

•Polisi wanataka kumweka kizuizini kwa uchunguzi zaidi kwa madai kuwa alitoa maneno ambayo huenda yakasababisha vurugu au kuyumbisha taifa.

•Ombi hilo linasomeka zaidi kwamba Odhiambo anaweza kutoroka.

mbele ya hakimu Gilbert Shikwe alifikishwa katika Mahakama ya Milimani kwa matamshi ya uchochezi aliyoyatoa wakati wa mkutano wa Azimio Jumapili Januari 31.
MCA wa Korogocho Absalom Odhiambo mbele ya hakimu Gilbert Shikwe alifikishwa katika Mahakama ya Milimani kwa matamshi ya uchochezi aliyoyatoa wakati wa mkutano wa Azimio Jumapili Januari 31.
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mwakilishi Wadi wa Korogocho, Absalom Odhiambo amefikishwa mbele ya mahakama ya Nairobi asubuhi ya leo Jumanne ambapo polisi wanatazamia kumzuilia kwa siku saba kutokana na matamshi ya uchochezi.

Katika ombi hilo ambalo bado halijasikilizwa, polisi wanataka kumweka kizuizini kwa uchunguzi zaidi kwa madai kuwa alitoa maneno ambayo huenda yakasababisha vurugu au kuyumbisha taifa.

Anadaiwa kutamka maneno hayo wakati wa mkutano wa Azimio wiki iliyopita katika Chungwa, House, Capitol Hill.

"Kwa siasa ya Taifa tunataka tutoke kwenda ikulu tutoe huyu mwizi, nataka tuingie town tufunge biashara, hakuna biashara itaendelea town ya Nairobi, ndio William Ruto aheshimu Raila Odinga. Lazima tufunge biashara hii town", ombi hilo linasoma

Polisi wanasema kwamba wanahitaji siku saba kupata uchochezi wowote unaowezekana, jumbe kutoka kwa simu yake na kurekodi taarifa kwa serikali ili kuongeza ushahidi kwa upande wa mashtaka.

Ombi hilo linasomeka zaidi kwamba Odhiambo anaweza kutoroka.