Idadi ya waliofariki katika ajali ya basi la Chuo cha Pwani wafika 17

Watu 12 walifariki papo hapo huku wawili wakiaga dunia wakipelekwa hospitalini siku ya Alhamisi.

Muhtasari

• Watu kadhaa walionusurika na majeraha wamelazwa katika vituo vya afya vya karibu huku wengine wakihamishiwa hospitali kuu ya Kenyatta. 

limehusika katika ajali Naivasha
Basi la Pwani University limehusika katika ajali Naivasha
Image: GEORGE MURAGE

Idadi ya waliofariki katika ajali ya Naivasha iliyohusisha basi la chuo kikuu cha Pwani imeongezeka hadi 17 baada ya wagonjwa wengine watatu kuaga kutokana na majeraha waliopata.  

Basi hilo lililokuwa likiteremka lilikuwa linawacha taa na kupiga honi kuonyesha tahadhari kabla ya kugonga matatu katika eneo la Kayole siku ya Alhamisi alasiri.  

Watu 12 walifariki papo hapo huku wawili wakiaga dunia wakipelekwa hospitalini siku ya Alhamisi.

Basi la chuo kikuu cha Pwani lilikuwa limebeba zaidi ya watu 30 wakati lilipogonga matatu kutoka nyuma kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.

Watu kadhaa walionusurika na majeraha wamelazwa katika vituo vya afya vya karibu huku wengine wakihamishiwa hospitali kuu ya Kenyatta. 

Mkuu wa polisi wa Bonde la Ufa, Tom Odera alisema dereva wa basi hilo alipoteza mwelekeo na kugonga takriban magari matano kabla ya kubingiria kwenye mtaro.

Manusura walisema kuwa huenda basi hilo lilipoteza breki kwani dereva aliambia kila mtu kufunga mshipi muda mfupi kabla ya ajali kutokea.