Kioni asisitiza kuwa kongamano la Jubilee litaendelea kama ilivyopangwa

Kaimu afisa mkuu mtendaji wa chama hicho Polycarp Hinga alisema NDC itaendelea kama ilivyopangwa Mei 22.

Muhtasari

• Taarifa ya katibu mkuu Jeremiah Kioni ilisema chama hicho kina wanachama wake wanaojulikana na hakikusanyi pesa kwa ajili ya shughuli hiyo.

 

JEREMIAH KIONI
Image: ENOS TECHE

Chama cha Jubilee sasa kinasisitiza kuwa Kongamano la Wajumbe wa Kitaifa lililopangwa bado linaendelea.

Katika taarifa yake, kaimu mkurugenzi mtendaji wa chama hicho Polycarp Hinga alisema NDC itaendelea kama ilivyopangwa Mei 22.

"Usichochwe urambwe, 1. @JubileePartyK NDC yetu inaendelea, kama ilivyoratibiwa tarehe 22 Mei. 2. Jihadhari na wahusika wachafu huko nje," alisema.

Hinga, hata hivyo, hakuzungumzia suala la ukumbi utakaoandaa.

Chama hicho pia kimewaonya wananchi dhidi ya kulaghaiwa pesa na watu wasiojulikana ambao inadaiwa wamekuwa wakiomba watu walipe ili wajumuishwe kuwa wajumbe wa chama hicho.

Taarifa ya katibu mkuu Jeremiah Kioni ilisema chama hicho kina wanachama wake wanaojulikana na hakikusanyi pesa kwa ajili ya shughuli hiyo.

"Wengine wanakusanya pesa kutoka kwa watu wasio na hatia kwa ahadi ya 'kuwajumuisha kama wajumbe," Kioni alisema.

"Tafadhali kumbuka kuwa kama chama, hatuhusiki katika mchango wowote wa majina au pesa kwa ajili ya NDC. Wajumbe wetu wa Jubilee Party wanajulikana na chama na wataalikwa kwa mpangilio mzuri. Usikubali ulaghai huu, "aliongeza.

Haya yanajiri saa chache baada ya kuchipuka kwa barua inayodaiwa kutoka Bomas of Kenya kunyima chama hicho nafasi ya kutumia ukumbi wake kwa kongamano la NDC.

Image: Maktaba

Barua hiyo ilidai kuwa ukumbi wa Bomas utakuwa unafanyiwa ukarabati na hivyo hauwezi kutumiwa kwa shughuli zozote.

" Ukumbi wetu mkuu, ambao uwezo wake ni watu 2,000, umepangwa kufanyiwa ukarabati kuanzia tarehe 16 Mei 2023 kwa muda wa wiki nane (8)," ilisema taarifa hiyo kwa kaimu mkurugenzi mtendaji Polycarp Hinga.

Barua hiyo iliongeza kuwa nafasi zingine ndani ya Bomas pia zimehifadhiwa kikamilifu kwa siku zijazo.

"Kwa kuzingatia maelezo hayo, kwa masikitiko yetu hatuwezi kuandaa NDC yenu tarehe 22 Mei 2023."

Juhudi za Meza yetu ya habari kumpata Polycarp Hinga wa Jubilee ili atoe maoni yake hazikufua dafu, kwani hakujibu simu.

Kiongozi wa chama cha Jubilee Uhuru Kenyatta mnamo Aprili 29 aliitisha Kongamano la Kitaifa la Wajumbe.

Wito huo ulitolewa huku kukiwa na mizozo kati ya pande mbili za chama hicho, kimoja kikiongozwa na katibu mkuu anayepigania wadhifa huo na mbunge wa EALA, Kanini Kega.

Kega anadai kuwa kaimu katibu mkuuna anaungwa mkono Rais William Ruto.

Katika notisi ya gazeti la serikali, Uhuru alisema pia watapokea ripoti ya hali kutoka kwa Kamati Kuu ya Kitaifa wakati wa kongamano hilo.