Ajali ya mashua Ziwani Victoria, watu 5 wasakwa huku 6 wakiokolewa

Wakati wa ajali hiyo mashua ilikuwa imebeba watu 11, magunia 100 ya makaa na magunia 40 ya samaki.

Muhtasari

• Ajali sawia ilitokea katika ziwa hilo Jumanne jioni wakati boti iliyokuwa ikisafirisha shehena ya vyakula kutoka visiwa vya Kasi kuelekea Katosi wilayani Mukono kupinduka ikiwa na mwanamume na mwanamke.

Wavuvi katika Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Koginga huko Homa Bay Picha: MAKTABA.
Wavuvi katika Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Koginga huko Homa Bay Picha: MAKTABA.

Shughuli ya uokoaji inaendelea katika Ziwa Victoria baada ya mashua iliyokuwa imebeba watu 11 na mizigo kuzama katika ziwa hilo.

Kulingana na duru za polisi mashua hiyo pia ilikuwa imebeba magunia 100 ya makaa, magunia 40 ya samaki na bidhaa za  binafsi ajali hiyo ilipotokea  siku ya Jumatano.

Mashua hiyo ilikuwa ikitoka visiwa vya Kiseba kuelekea Katosi huko Mukono. Ilipinduka kati ya Jana na Kumi lakini muda kamili wa ajali hiyo haujajulikana.

Watu sita waliokolewa na boti nyingine ya usafiri, lakini watu watano bado hawajulikani waliko na polisi wa majini walikuwa wakiendesha operesheni ziwani kuwatafuta.

Ajali sawia ilitokea katika ziwa hilo Jumanne jioni wakati boti iliyokuwa ikisafirisha shehena ya vyakula kutoka visiwa vya Kasi kuelekea Katosi wilayani Mukono kupinduka ikiwa na mwanamume na mwanamke.

Mwanamke huyo alikufa maji huku mwanamume akiokolewa na wafanyabiashara wa samaki.

Polisi walisema huenda mashua hizo zilizama kutokana na kubeba mzigo kupita kiasi.