Peter Kaluma: Wapenzi wa jinsia moja kufugwa miaka 50

Pigo kwa wapenzi wa jinsia moja iwapo mbunge itaidhinisha mswanda

Muhtasari

•Tunaendelea kuhimiza Mahakama ya Juu ya Kenya kufikiria kurekebisha uamuzi ulioruhusu LGBTQ kusajili chama chao.

•Tayari tunawaona watoto wetu wa shule za msingi, sekondari na vyuo wakijishughulisha na vitendo hivi visivyo vya kimungu kwa madhara ya kizazi kijacho.

PETER KALUMA
Image: HISANI

Unaweza kutumikia kifungo cha nusu karne endapo utapatikana kwa mapenzi ya jinsia moja endapo bunge litaidhinisha mswada uliopelekwa na mbunge wa Homabay Peter Kalume kuwa sheria.

Ili kulinda maadili ya mswada wa sheria wa ulinzi wa familia2023 unaofadhiliwa na Kaluma unapendekeza kupiga marufuku ndoa za jinsia moja na ushawishi wowote wa LGBTQ na ushawishi wake

Mswanda huu ulio mbele ya kamati ya idara ya ulinzi ya kijamii pia hunaaramisha mikutano ya gwaride ya mashonga na maandamano barabarani na vile vile mavazi yao hadharani

Kulingana na mbunge wa homabay town, ngono inasalia kuwa hali ya kihisia ya kuwa mwanamume au mwanamke inayozingatiwa wakati wa kuzaliwa

Kanisa pia linaunga mkono kwa Mswada wa Kaluma, unaolenga kuendeleza masharti ya Ibara ya 45 ya Katiba inayotoa ulinzi wa familia, kukataza na kuharamisha ushoga, ndoa za jinsia moja, vitendo vya ngono kinyume cha asili na shughuli zinazohusiana nazo.

Yote ni kinyume na maadili ya umma. Mswada huo, ambao pia unalenga kudhibiti shughuli au vyama vinavyotaka kuendeleza, kutetea au kuendeleza ushoga, vitendo vya ngono visivyo vya asili na uhusiano wa kingono usio wa pande mbili, unapaswa kuungwa mkono na wajumbe wote wa Bunge la Kitaifa na pia maseneta kulingana na makasisi umu nchini

Mbunge kaluma anapingia debe muswanda huu na iwapo utapitishwa utaanza kufanya kazi mara moja kulingana na yeye aidha wapenzi wa jinsia moja wanazindi kulamikia haki yao .