Mshukiwa wa mauaji ya Eric Maigo sio mtoto ana umri kujibu mashtaka

Alikamatwa katika eneo la Olympic mtaani Kibra baada ya wananchi kuarifu polisi kuhusu alikokuwa.

Muhtasari

• Adhiambo anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Maigo ambaye mwili wake ulipatikana nyumbani kwake ukiwa na majeraha 25 ya kuchomwa kisu

Mwanamke asakwa na DCI kuhusiana na mauaji ya mkurugenzi wa  fedha wa Nairobi hospital
Image: DCI/X

Anne Adhiambo Akinyi, mshukiwa mkuu wa mauaji ya kinyama ya Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Hospitali ya Nairobi Eric Maigo yuko tayari kujibu mashtaka.

Haya yaliibuka siku ya Jumatano kufuatia tathmini ya umri na kiakili iliyofanywa katika Hospitali ya Mathare jijini Nairobi ambayo ilithibitisha kuwa yeye ni Mkenya mzima mwenye akili timamu kinyume na ripoti za awali kwamba huenda alikuwa mtoto.

Adhiambo aliwasilishwa mbele ya mahakama kwa maombi mengine tofauti mnamo tarehe 27 Septemba, ambapo mahakama iliupa upande wa mashtaka siku 21 kumshikilia akisubiri kukamilika kwa upelelezi.

Mtu aliyeaminika kuwa Adhiambo alinaswa kwenye CCTV akitoroka eneo la mauaji ya Maigo asubuhi ya tarehe 15 Oktoba katika mtaa wa Jamhuri, Nairobi.

Alikamatwa katika eneo la Olympic mtaani Kibra baada ya wananchi kuarifu polisi kuhusu alikokuwa.

Adhiambo anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Maigo ambaye mwili wake ulipatikana nyumbani kwake ukiwa na majeraha 25 ya kuchomwa kisu, mshukiwa anatarajiwa mahakamani tarehe 28 Oktoba.