Polisi wamuua mshukiwa mmoja wa Al-Shabaab Garissa

Polisi wasema kuwa wameongeza oparesheni za kuwasaka wanamgambo katika Kaunti ya Garissa

Muhtasari

•Hili ni tukio la hivi punde zaidi kutokea katika eneo hilo,Maafisa walisema wengi wa magaidi hao walikuwa wameweka kambi huko Garissa ambazo wamekuwa wakizitumia kufanya mashambulizi dhidi ya madereva na magari ya serikali

Maafisa wa usalama walivamia  kambi ya muda ya al-Shabaab huko Dabalwein  Kaunti ya Garissa na kumuua mwanamgambo mmoja, Idadi isiyojulikana ya washukiwa walitoroka na majeraha katika uvamizi huo wa Jumanne jioni, polisi walisema.

Kiokosi hicho cha poisi kilifanikiwa kupata bunduki za AK47, risasi 90, dawa, vyakula, Pia walipata vifaa vya matibabu na vifaa vya kutengenezea Vilipuzi  polisi walisema.

Polisi walisema kuwa wameongeza oparesheni za kuwasaka wanamgambo hao katika Kaunti ya Garissa na kaunti zingine ili kuzuia mashambulio yaliyopangwa nchini.

Hili ni tukio la hivi punde zaidi kutokea katika eneo hilo,Maafisa walisema wengi wa magaidi hao walikuwa wameweka kambi huko Garissa ambazo wamekuwa wakizitumia kufanya mashambulizi dhidi ya madereva na magari ya serikali.

Mnamo Novemba 4, wanachama wawili wa kundi la kigaidi waliokuwa wakihudumu kama madaktari wa kundi hilo waliuawa katika uvamizi wa polisi katika kambi yao huko Fafi, Kaunti ya Garissa.

Polisi walisema kisa hicho kilitokea katika kambi ya matibabu ya genge hilo katika eneo la Hagarso.

Madaktari hao Wawili waliouawa wa al Shabaab walikuwa wakiwatibu wanamgambo waliojeruhiwa na mashirika ya usalama.

Polisi wamefuatilia baadhi ya dawa zilizopatikana katika hospitali moja mjini Garissa huku Wamiliki wa hospitali hiyo wakiwekwa chini ya uchunguzi.

 Vikosi vya usalama katika eneo hilo pia mwezi uliopita viliharibu kambi ya vifaa iliyokuwa ikitumiwa na wanamgambo wa al Shabaab huko Dahun na Fafi, kaunti ya Garissa na kupata vyakula vya aina mbalimbali.

Operesheni hiyo ya polisi  ilipata mchele, sukari na maji,Maafisa hao waliharibu vyakula hivyo na kuendelea kuwafuata magaidi waliokuwa wakitumia kituo hicho.