Gilad awaruhusu wanawe kuondoka Kenya kujiunga na jeshi la Israel kupambana na Hamas

Huko Gaza, Wizara ya Afya ilisema Jumamosi kwamba mashambulizi ya anga ya Israel yameua watu wasiopungua 2,215, wakiwemo watoto 724, na kuwaacha zaidi ya wengine 8,714 kujeruhiwa.

Muhtasari

• "Alipokelewa uwanja wa ndege asubuhi ya leo na dada yake Lia ambaye ni mwanajeshi IDF," Gilad alifichua.

• Gilad ni raia wa Israel ambaye pia hivi majuzi amepata uraia wa Kenya na ni mkulima shupavu wa vitunguu katika kaunti ya Kajiado.

Wanawe Gilad waondoka kwenda Israel kupambana na Hamas
Wanawe Gilad waondoka kwenda Israel kupambana na Hamas
Image: Facebook

Msanii na mkulima wa vitunguu maarufu wa Kenya, Gilad ambaye pia ni raia wa Israel aliyechagua kuhamia na kupata uraia wa Kenya kabisa amewashangaza mashabiki wake kwa kufichua kwamba wanawe wawili wameondoka kwenda Israel kupambana na kundi la kigaidi la Hamas.

Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Gilad alisema kwamba wanawe wawili walizaliwa Kenya lakini wamefanya uamuzi wa kwenda katika nchi ya kuzaliwa ya baba yao ili kujiunga na jeshi la Israel katika kuipambani bendera yake katika vita vinavyoendelea vya Israel na kundi la itikadi kadi la Kipalestina, Hamas katika ukanda wa Gaza.

Kwa faraja, Gilad alifichua kwamba bintiye tayari ni mwanajeshi wa Israel na mvulana wake alimaliza mafunzo ya jeshi mwaka mmoja uliopita na amekuwa akijifunza binafsi nchini Nicaragua hadi pale aliposikia kuhusu mauaji ya kimbari ambayo Hamas walitekeleza kwa watu wa Israel Jumamosi iliyopita.

“Mapema asubuhi ya leo mwana wetu Omer alitua Israel kujiunga na kikosi chake cha askari kama askari wa akiba katika Jeshi la Ulinzi la Israel. Omer ambaye alimaliza utumishi wake wa jeshi zaidi ya mwaka mmoja uliopita alikuwa akijivinjari nchini Nicaragua mnamo Oktoba 7 wakati magaidi wa Hamas waliwaua zaidi ya Waisraeli 1300 wasio na hatia 💔. Bila kusita na licha ya kukatishwa safari nyingi alipata njia ya kufika nyumbani Israel na kupokelewa uwanja wa ndege asubuhi ya leo na dada yake Lia ambaye ni mwanajeshi IDF na amekuwa akifanya kazi usiku na mchana tangu unyama wa Jumamosi asubuhi,” Gilad alidokeza.

Gilad aliwatakia wanawe wote kila la heri katika kupambania Israel katika mzozo huo ambao Hamas waliuwa Zaidi ya Waisrael 1200 baada ya shambulizi la kushtukiza kwenye hafla ya muziki Jumamosi ya Oktoba 7.

“Watoto wetu wote wawili walikulia nchini Kenya na walichagua kujiunga na jeshi la Israel kwa sababu ya wajibu na wote wawili wamepoteza watu wanaowajua katika mashambulizi haya ya kutisha kama vile marafiki zao wote walivyofanya 💔 Watoto na mimi na Mama yako tunajivunia. Mzazi yeyote anaweza kuwa wa watoto wao kwa binadamu wa ajabu mmekuwa ❤️ mioyo yetu imejaa. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awaweke salama na afya njema,” alisema.

Huko Gaza, Wizara ya Afya ilisema Jumamosi kwamba mashambulizi ya anga ya Israel yameua watu wasiopungua 2,215, wakiwemo watoto 724, na kuwaacha zaidi ya wengine 8,714 kujeruhiwa.