KCPE 2023:Matokeo ya KCPE na KPSEA kutangazwa leo

Zaidi ya watahiniwa milioni 1.4 walifanya mtihani ya KCPE idadi kubwa zaidi kulinganishwa na mwaka jana ambapo watahiniwa 1,244,188 walisajiliwa kufanya mitihani hiyo

Muhtasari

• Kundi la 2023 lilikuwa la mwisho kufanya mitihani ya KCPE huku wizara ikijishughulisha na kumaliza mtaala wa 8-4-4.

•Machogu alipokuwa akizungumza Jumanne jijini Nairobi alisema mtihani huo ambao ulifanywa kati ya Oktoba 30 na Novemba 1 ulihitimishwa vyema.

Waziri wa Elimu,Ezekiel Machogu
Waziri wa Elimu,Ezekiel Machogu
Image: HISANI

Matokeo ya mitihani ya kitaifa ya KCPE na KPSEA  yatatolewa Alhamisi, Novemba 23, 2023.

Taarifa kutoka kwa Wizara ya Elimu ilisema hafla hiyo itasimamiwa na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu katika Jumba jipya la Baraza la Mitihani nchini Kenya mtaani South  C.

Kundi la 2023 lilikuwa la mwisho kufanya mitihani ya KCPE huku wizara ikijishughulisha na kumaliza mtaala wa 8-4-4.

Mwaka huu, zaidi ya watahiniwa milioni 1.4 walifanya mtihani ya KCPE idadi kubwa zaidi kulinganishwa na mwaka jana ambapo watahiniwa  1,244,188 walisajiliwa kufanya mitihani hiyo huku watahiniwa milioni 1.2 wakifanya mitihani ya KPSEA.

Machogu alisema kuwa watahiniwa watajulishwa shule watakazo jiunga nazo kabla ya sherehe za Krisimasi

Machogu alipokuwa akizungumza Jumanne jijini Nairobi alisema mtihani huo ambao ulifanywa kati ya Oktoba 30 na Novemba 1 ulihitimishwa vyema.

"Hakukuwa na kesi za udanganyifu. Hakuna kesi za utovu wa nidhamu. Tulikuwa na kesi sita tu ambazo zilikuwa za kujaribu kudanganya. Kati ya watahiniwa 1,415,315, kesi tuliokuwa nazo zilikuwa sita," alisema.

Wakati wa kutolewa kwa matokeo ya KCPE ya mwaka jana, Machogu alisema kulikuwa na visa 252 vya makosa ya mtihani.

Alisema watahiniwa hao walinaswa wakijihusisha na visa vya wizi wa mitihani katika vituo tisa vya kufanyia mitihani.

Hata hivyo watahiniwa hao hawakutunukiwa alama zozote katika masomo waliyojihusisha na utovu wa nidhamu, CS alisema basi.

"Kwa ujumla, watahiniwa 252 katika vituo tisa walibainika kujihusisha na makosa. Watahiniwa hawa wamepata sifuri katika masomo waliyofanya utovu wa nidhamu. Hata hivyo, alama za jumla za wanafunzi walioathirika zitakokotolewa chini ya alama walizopewa." walioathirika,” alisema wakati akitoa matokeo Desemba 21, 2022.