Wasimamizi na wasahishaji wa mtihani KCPE tayari wamelipwa -Kipsang

Kwa mara ya kwanza wasimamizi wa mtihani walipwa kwa wakati ufaao katibu asema

Muhtasari

•Mitihani ya mwaka huu ilivutia watahiniwa milioni 1,406,557,huku Kundi la 2023 lilikuwa la mwisho kufanya mitihani ya KCPE,kumaliza mtaala wa 8-4-4

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu na Katibu wa Idara ya Elimu ya Msingi Belio Kipsang
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu na Katibu wa Idara ya Elimu ya Msingi Belio Kipsang

Katibu Mkuu wa Elimu Belio Kipsang amethibitisha kuwa wasimaminzi na wasahishaji wa mtihani wa KCPE  mwaka huu  tayari wamelipwa.

Belio alisema wizara  ya elimu ina rasilimali za kutosha kuwalipa wataalamu ambao wamekuwa wakishughulikia mitihani hiyo.

"Tunataka kuwahakikishia walimu wetu kwamba mwaka huu, tutaweza kulipa malipo yote ambayo yanadaiwa kwa wakati ufaao," alisema.

Akizungumza wakati wa kutolewa kwa mtihani wa KCPE wa 2023 katika Jumba la Mitihani jijini Nairobi, katibu huyo alisema  kuwa hata wasimaminzi na wasahishaji wa mtihani wa KCSE watalipwa kwa wakati.

“Ninataka kuwahakikishia wahusika  wote wa  mtihani wa KCSE kwamba tutahakikisha wanalipwa kwa wakati,” Kipsang alisema

Baada ya kukamilika kwa mitihani ya KCPE mnamo Novemba 1, alisema kusahihisha kulitaanza mara moja ili kuwaruhusu wazazi kupata matokeo ya watoto wao kabla ya msimu wa sherehe.

"Kabla hatujaadhimisha Krismasi, wazazi wetu watajua ni wapi watoto wao watapata nafasi ya kuendeleza masomo yao kwenye shule za upili," Kipsang alisema.

Katibu huyo alisemakuwa  kabla ya mwisho wa Januari 2024, kila mwanafunzi anapaswa kuwa shuleni.

Mitihani ya mwaka huu ilivutia watahiniwa milioni 1,406,557,huku Kundi la 2023 lilikuwa la mwisho kufanya mitihani ya KCPE,kumaliza mtaala wa 8-4-4.