Watu 3,609 wamefariki kutokana na ajali ya barabarani mwaka wa 2023 - NTSA

Katika ripoti yao ya hali ya Usalama Barabarani ya Oktoba, NTSA ilisema Januari ilirekodi vifo 379, Februari ilikuwa na 340, Machi 389, Aprili 357 na Mei ilikuwa na 340.

Muhtasari

• Idadi hii ya vifo imetokana  ya kuanzia mwezi wa Januari  hadi Oktoba 2023.

• Mnamo 2022, takriban watu 4,690 walipoteza maisha kwenye ajali za  barabarani nchini

Ajali ya barabarani
Ajali ya barabarani
Image: Hisani

Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA) imefichua kuwa watu 3,609 walipoteza maisha yao katika ajali za barabarani mnamo 2023.

Idadi hii ya vifo imetokana  ya kuanzia mwezi wa Januari  hadi Oktoba 2023.

Hii, hata hivyo, ni kushuka kwa idadi ya vifo katika kipindi kama hicho mwaka jana, ambacho kilisimama kwa 3,936. Hili lilikuwa punguzo la asilimia 8.31.

Katika ripoti yao ya hali ya Usalama Barabarani ya Oktoba, NTSA ilisema Januari ilirekodi vifo 379, Februari  ilikuwa na 340, Machi 389, Aprili 357 na Mei ilikuwa na 340.

Juni ilirekodi vifo 439, Julai  325, Agosti  327, huku Septemba  na  Oktoba zikiripoti vifo 330 na 338 mtawalia.

Mnamo 2022, takriban watu 4,690 walipoteza maisha kwenye ajali za  barabarani nchini.

Mwaka huo ulirekodi vifo vya ajali za barabarani 21,757, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.5 kutoka ile iliyoripotiwa mwaka 2021.

Idadi ya wahasiriwa waliopata majeraha mabaya mnamo 2022 ilikuwa 9,935, wakati waliopata majeraha kidogo mnamo 2022 waliongezeka kutoka 1,136 hadi 7,132.

Wanaotembea kwa miguu ndio walioandikisha vifo vingi zaidi vya 1,682 huku waendesha pikipiki wakiwa 1,254.

Madereva walikuwa 426, abiria 822, pilioni abiria 445 na wapanda baiskeli  61.

Vifo vya abiria viliongezeka kutoka waathiriwa 7,586 mwaka 2021 hadi 9,161 mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20.8.

Kulingana na NTSA, sababu kuu za ajali mbaya mnamo 2022 ni pamoja na kugonga-na-kimbia, kupasuka kwa matairi, na, magari na pikipiki kukosa udhibiti.

Pia kupita njia isivyofaa na kushindwa kushika njia ifaayo na kusababisha migongano ya uso kwa uso zilitajwa kuwa sababu.